Pata taarifa kuu
BURKINA FASO

Burkina Faso yarejesha katiba, makubaliano ya serikali ya mpito kusainiwa leo

Kiongozi wa sasa wa Burkina Faso, Luteni Kanali Isaac Zida ametangaza leo Jumamosi kurejesha matumizi ya Katiba aliyokuwa amesitisha baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Blaise Compaoré, hatua muhimu katika kutatua mgogoro nchini humo. 

Luteni Kanali Isaac Zida akiwa  Ouagadougou, nchini  Burkina Faso,tarehe 14 Novemba 2014.
Luteni Kanali Isaac Zida akiwa Ouagadougou, nchini Burkina Faso,tarehe 14 Novemba 2014. ISSOUF SANOG / AFP
Matangazo ya kibiashara

Luteni Kanali Zida amesema kuwa kurejeshwa kwa katiba ya tarehe 2 mwezi Juni mwaka 1991 kunalenga kufanikisha mchakato wa kuunda serikali ya kiraia na kutazamia kurejea kwa maisha ya kawaida ya kikatiba.

Marejesho ya Sheria ya Msingi ni hatua muhimu nchini Burkina Faso kwa vile itafungua mlango kwa mapitio ya Baraza la Katiba ya mkataba wa mpito, ambao utatiliwa saini rasmi kesho Jumapili ambapo mara baada ya kupitishwa na Baraza, itakuwa kama msingi wa kitaasisi kwa ajili ya serikali ya mpito ya Burkina Faso.

Aidha Luteni Kanali Zida amewaalika wajumbe wa makundi yote ya kiraia yaliyoshiriki mchakato wa mpito kupeleka majina ya wagombea wao wa urais wa mwaka 2015 hadi kufikia kesho saa sita mchana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.