Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIMONE-SHERIA

Simone Gbagbo mbele ya majaji

Kwa muda wa miezi miwili, baada ya kuanza kusikilizwa kesi inayowahusu viongozi waliohusika na vurugu katika utawala wa laurent Gbagbo, sasa mke wa rais huyo wa zamani wa Côte d’Ivoire Simone Gbagbo anatazamiwa kusikilizwa mahakamani Jumatatu wiki hii.

Simone Gbagbo, mke wa rais wa aliyekua rais wa Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo. Kwa mujibu wa wanasheria wake, Simone Gbagbo anasubiri kuripoti mbele ya majaji ili kujua anachotuhumiwa.
Simone Gbagbo, mke wa rais wa aliyekua rais wa Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo. Kwa mujibu wa wanasheria wake, Simone Gbagbo anasubiri kuripoti mbele ya majaji ili kujua anachotuhumiwa. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Simone Gbagbo anatuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa. Uhalifu uliyotekelezwa wakati wa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi, kati ya miaka ya 2010 na 2011. Machafuko ambayo yaligharimu maisha ya watu takribani 3000 kutoka pande zote zilizokua zikihasimiana.

Baada ya kusikilizwa kwa mawaziri kadhaa katika utawala wa Laurent Gbagbo pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa viliyokua vikishirikiana na utawala wakati huo, ni wakati sasa wa Simone Gbagbo kusikilizwa na vyombo vya sheria vya Côte d’Ivoire.

Mmoja kati ya wanasheria wa Simone Gbagbo, Habiba Touré, amewasihi baadhi ya watu ambao wamekua wakithibitisha kwamba mteja wao alihusika katika machafuko yaliotokea katika miaka ya 2010 na 2011 nchini Côte d’Ivoire.

“ Unaweza ukasema kuwa hauhusiki katika makosa unayotuhumiwa bila hata hivyo kufanya vitisho. Kwa hiyo Simone Gbagbo ataweka wazi ukweli wake. Na upande wa mashitaka utatoa ushahidi wake”, amesema Habiba Touré

Simone Gbagbo hajajieleza hadharani tangu alipokamatwa Aprili 11 mwaka 2011 mjini Abidjan pamoja na mumewe Laurent Gbagbo. Kwa mujibu wa wanasheria wake, Simone Gbagbo ana mengi ya kuongea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.