Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-USALAMA

Siku ngumu kwa kesi ya Simone Gabgbo

Kesi ya mke wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo, Simone Gbagbo, ambaye anatuhumiwa " kuhatarisha usalama wa taifa", imesikilizwa kwa mara nyingine tena Jumatatu Desemba 29 mwaka 2014.

Desemba 26, kizimbani, Simone Gbagbo ameonekana kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake pamoja na mumewe mwezi Aprili mwaka 2011.Waziri Mkuu wa zamani Gilbert Ake N'Gbo (kulia) pia anatuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa.
Desemba 26, kizimbani, Simone Gbagbo ameonekana kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake pamoja na mumewe mwezi Aprili mwaka 2011.Waziri Mkuu wa zamani Gilbert Ake N'Gbo (kulia) pia anatuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo imesikilizwa kufuatia malalamiko ya ndugu wa waliouawa katika machafuko yaliotokea katika miaka ya 2010 na 2011 nchini Cote d'Ivoire, ambao wamekua wakiomba watendewe haki.

Simone Gbagbo, mwenye umri wa miaka 65, akijulikana kwa jina la "mwanamke mwenye nguvu" alishitakiwa pamoja na viongozi wengine 82 waliokua wakishikilia nyadhifa mbalimbali katika utawala wa Laurent Gbagbo.

Kesi hii imesikilizwa jana Jumatatu Desemba 29 kwa mara ya pili baada ya ufunguzi Ijumaa Desemba 26 kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa. Simone Gbagbo na viongozi wengine 82 wanakabiliwa na tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa.

Kesi hii ilianza kusikilizwa katika mji mkuu wa Cote d'Ivoire, Abidjan wakati serikali ya rais Alassane Ouattara ikikataa kumuhamisha Simone Gbagbo kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ambayo inamtuhumu kuhusika makosa ya " uhalifu dhidi ya ubinadamu", kama mume wake, anayezuiliwa miaka mitatu katika jela za ICC, mjini The Hague.

Washitakiwa watapaswa kujibu mashtaka ya uhalifu uliotekelezwa kati ya mwaka 2010 na 2011, wakati wa machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi, machafuko ambayo yalisababisha vifo vya watu 3,000 kwa pande zote husika.

Kesi hii inaendelea kwa siku ya tatu leo Jumanne Desemba 30.

Wakati huo huo kesi nyingine ya pili inayohusu kugombea kwa rais wa zamani Laurent Gbagbo katika uongozi wa chama imesikilizwa Jumatatu Desemba 29.

Mahakama imechukua uamzi wa kutokubali pendekezo lolote la kugombea kwa Laurent Gbagbo katika uongozi wa chama cha FPI

Wanasheria wa Laurent Gbagbo wamesema watakata rufaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.