Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-AFYA

Jean-Claude Muyambo akabiliwa na hatari ya kukatwa mguu

Wakili Jean-Claude Muyambo akiwa pia mwenyekiti wa chama cha upinzani cha SCODE nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo alieko kizuwizini mjini Kinshasa anakabiliwa na hatari ya kukatwa mguu wake wa kushoto na kuishia kuwa mlemavu kulingana na Daktari wake.

Mwenyekiti wa chama cha mawakili DRC, Jean-Claude Muyambo (akiwa na kipaza sauti)  2007.
Mwenyekiti wa chama cha mawakili DRC, Jean-Claude Muyambo (akiwa na kipaza sauti) 2007. AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Daktari Steeve Makolo ameyasema hayo hapo Jumanne wiki hii mjini Kinshasa akibainisha kuwa mifupa ya mguu wa mteja wake imesagwa kufuatia mateso aliyoyapata wakati alipokamatwa katika muktadha wa maandamano ya mwezi Januari mjini Kinshasa.

Aidha, Dk Makolo amechambua picha ya Kliniki ya Jean-Claude Muyambo na kutaka mwanasiasa huyo ahamishwe haraka iwezekanavyo katika hospitali maalum nje ya nchi ili kuepuka kukatwa mguu kwa vile kulingana naye hali ya mguu huo si nzuri.

Kulingana na daktari huyo, Jean-Claude Muyambo sasa anatembea kwa kutegemea magongo, huku akikabiliwa na maumivu makali ya mguu wake huo.

Jean-Claude Muyambo anatuhumiwa na mwendesha mashitaka wa Mahakama ya mjini Lubumbashi kwa ubadhirifu na ulaghai kwa kuuza mali ya mteja wake bila ya hati ya umiliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.