Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

DRC: wafuasi wa chama cha UNAFEC wakamatwa Lubumbashi

Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji Jumanne wiki hii mjini Lubumbashi, mkowa wa Katanga.

Picha ya kiongozi wa chama cha UNAFEC, Antoine Gabriel Kyungu Wa Kumwanza mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa urais , Lubumbashi, Mei 29, 2015.
Picha ya kiongozi wa chama cha UNAFEC, Antoine Gabriel Kyungu Wa Kumwanza mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa urais , Lubumbashi, Mei 29, 2015. AFP PHOTO/FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wamethibitisha kuwa watu wanane wameshikiliwa na polisi kufuatia kile walichosema ndio walioamuru vijana wao kuwarushia mawe.

Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi baada ya Rais wa chama cha UNAFEC, Gabriel Kyungu wa Kumwamza kuwataka vijana wafuasi wa chama chake kutokujiunga na maandamano yoyote mjini humo.

Vyanzo kutoka mjini Lubumbashi vinasema kuwa wafuasi wa chama hicho walikuwa wamekusanyika kwenye ofisi yao wakiongozwa na kinara wao Kabulo Shimbe Zasou, ghafla wakakamatwa na polisi na hadi wakati huu bado wanazuiliwa.

Ifahamike kuwa, chama hicho cha UNAFEC kilibanduliwa kutoka muungano unaoongoza nchini DRC, kwa kudai kuwa Rais Joseph Kabila anapania kusalia madarakani hata baada ya kumaliza muhula wake mwaka ujao wa 2016.

Hayo yakijiri Katibu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI Bi. Chantal Ngoyi Tshite Wetshi amejiuzulu kwenye waadhifa wake huo baada ya Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti.

Katika barua aliomwandikia Spika wa Bunge, Chantal Ngoyi ameelezea shinikizo alizozipata ili ajiuzulu kufuatia chama chake cha MSR kujiondoa kwenye muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Rais wa Congo Joseph kabila.

Akihijiwa na RFI, Msemaji wa Muungano huo Andre-Alain Atundu hakuficha kuridhishwa kwake na tangazo hilo la kujiuzulu kwa Bi. Chantal Ngoyi akibainisha kuwa nafasi ya Katibu ni ya vyama vinavyomuunga mkono rais Kabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.