Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Waziri Naledi Pandor aituhumu Israel kwa kumtishia

Nairobi – Waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini Naledi Pandor ameituhumu idara ya ujasusi ya Israeli kwa kile anachodai kuwa idara hiyo imekuwa ikimtishia kufuatia hatua yake ya kuwasilisha kesi katika mahakama ya ICJ kuhusu kinachoendelea Gaza.

 Naledi Pandor- Waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini
Naledi Pandor- Waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini © AFP - ATTA KENARE
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na majarida ya The Mail na The Guardian siku ya Alhamis, waziri huyo ameeleza kwamba ana wasiwasi kuhusu maisha yake na familia yake baada yake kulengwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa waziri huyo, tayari ametoa taarifa kwa mwenzake wa polisi nchini Afrika Kusini Bheki Cele kumuongezea ulinzi baada ya kupokea kile anchodai ni kupokea taarifa za vitisho.

Israel haijatoa taarifa kuhusu madai hayo ya waziri Pandor.
Israel haijatoa taarifa kuhusu madai hayo ya waziri Pandor. © PIROSCHKA VAN DE WOUW / Reuters

Israel haijatoa taarifa kuhusu madai hayo ya waziri Pandor.

Mwezi uliopita, mahakama ya ICJ katika uamuzi wake iliitaka nchi ya Israel kuchukua hatua za kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki dhidi ya raia wa Palestine katika ukanda wa Gaza na kutoa taarifa katika kipindi cha mwezi moja.

Afrika kusini ilikuwa imewasilisha kesi dhidi ya Israel katika mahakama ya ICJ ikiituhumu kwa kukiuka haki za binadamu katika mzozo unaoendelea huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.