Pata taarifa kuu
SIASA-UCHUMI

Afrika Kusini: Malema azindua kampeni ya EFF kwa uchaguzi mkuu

Kiongozi shupavu wa chama chenye siasa kali za mrengo wa kushoto cha Afrika Kusini, Julius Malema, amezindua kampeni za chama chake siku ya Jumamosi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, akikishutumu chama tawala cha ANC na kutishia kurudisha nyuma uchaguzi wa kihistoria, kwa kutochukua hatua katika kukabiliana na machafuko ya nchi hiyo.

EFF, ambayo imechochewa na Umaksi-Leninism, imeonyesha wazi kuunga mkono Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine mapema 2022.
EFF, ambayo imechochewa na Umaksi-Leninism, imeonyesha wazi kuunga mkono Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine mapema 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mbele ya maelfu ya wafuasi waliokusanyika katika uwanja karibu kujaa mjini Durban (mashariki), mji mkuu wa jimbo kuu la KwaZulu-Natal lenye idadi kubwa ya wapiga kura, kiongozi wa chama cha pili cha upinzani alikishutumu chama cha African National Congress (ANC) kwa "ubaguzi wa rangi katika suala la kiuchumi". "Uhuru bila ajira ni nini?", amesema, "uhuru bila umeme ni nini?"

Rais Cyril "Ramaphosa anaendelea kuua watu wetu," amesisitiza Bw. Malema, akiwa amevaa bereti yake nyekundu isiyoweza kuharibika na anayejulikana kwa uchochezi wake na maneno yake ya kushangaza. "Tunataka utawala wa kuutumia kwa uamuzi."

Nguvu kuu za kiviwanda katika bara hili zinakabiliwa na shida kubwa ya nishati na kusababisha kukatika kwa umeme hadi saa kumi na mbili kwa siku. Hali ya hewa ya kijamii na kiuchumi pia ina alama ya ukosefu wa ajira uliokithiri na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa. Katika muktadha huu wa huzuni na taswira iliyoharibiwa na kesi za ufisadi, ANC ikiwa kinara wa nchi tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi iko hatarini kupoteza wingi wake kamili Bungeni kwa mara ya kwanza kufuatia uchaguzi ujao, kulingana na tafiti za maoni.

Takriban Waafrika Kusini milioni 27.5 waliojiandikisha kupiga kura watalazimika kupiga kura kati ya mwezi Mei na Agosti kwa, kuwachaguwa wabunge waowapya, na bunge baadaye litamteua rais ajaye. Tarehe kamili ya uchaguzi bado haijatangazwa. Katika miezi ya hivi karibuni, vyama vya upinzani vimetafuta kikamilifu mikakati ya muungano ili kukiondoa chama cha ANC.

Chama cha kwanza, Democratic Alliance (DA), ambacho bado kinatambulika kama chama cha wazungu, kilianzisha muungano na makundi kumi madogo ya kisiasa. Ikisimamia jiji la Cape Town, DA, hata hivyo, ilikataa kwa uthabiti kusogea karibu na EFF, ikitoa mfano wa tofauti kubwa za "maadili na kanuni".

"Bwana wa Vita"

EFF, ambayo imechochewa na Umaksi-Leninism, imeonyesha wazi kuunga mkono Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine mwanzoni mwa mwaka 2022. Siku ya Jumamosi, Julius Malema, ambaye mara kwa mara anaandika vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari vya ndani kwa matembezi yake ya uchochezi, alimwita Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu "mbabe wa kivita".

Wabunge wa EFF hawakuhudhuria hotuba ya kila mwaka ya Rais Ramaphosa kuhusu hali ya taifa wiki hii. Mwaka jana, baadhi yao walivamia jukwaa na kukatiza hotuba ya mkuu wa nchi.

Licha ya mikikimikiki hiyo, umaarufu wa chama hicho unazidi kupanda na kinaweza kurejesha nafasi ya kuongoza vuguvugu la upinzani nchini. Kulingana na kura ya hivi majuzi ya Ipsos, EFF na DA zinalingana kwa karibu na 17% na 20% ya nia ya kupiga kura. Katika uchaguzi mkuu wa 2019, EFF ilipata zaidi ya 10% ya kura.

Malema ni maarufu kwa sababu amejidhihirisha kama mtu anayethubutu kupinga madaraka waziwazi," anasema mchambuzi wa kisiasa Sandile Swana. Na "EFF imeunda utambulisho kama chama cha vijana wasomi na wanafikra wanaotetea elimu ya watu weusi.

Katika miaka ya hivi karibuni, chama hicho kimejaribu kupanua wigo wake kwa kuwalenga vijana wa vyuo vikuu ambao wamekerwa na umaskini unaoongezeka. Julius Malema, ambaye ni mhusika wa kesi kadhaa za kisheria, mara kwa mara anaahidi ajira na elimu bila malipo kwa wote, pamoja na kurejesha ardhi kwa Waafrika Kusini weusi kwa kutumia hatua za kunyang'anywa bila fidia.

Malema, 42, alianzisha EFF mwaka wa 2013 baada ya kuondoka ANC, ambako aliongoza Umoja wa Vijana. Kwa sasa ANC ina viti 230 kati ya 400 (57.50%) katika Bunge la Kitaifa, DA 84 (20.77%) na EFF 44 (10.79%).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.