Pata taarifa kuu

Kupungua kwa misaada nchini Uganda: Utapiamlo unaongezeka katika kambi za wakimbizi wa Kongo

Wakikimbia takriban miaka 30 ya ghasia mashariki mwa DRC, Wakongo wengi wanachukua njia ya kukimbilia uhamishoi na hasa kuelekea nchi jirani ya Uganda, ambayo imesifiwa kwa kuwapokea wakimbizi wengi kutoka ukanda huo. Kila wiki, wakimbizi wapya kutoka Kongo wanawasili Nakivale, mojawapo ya kambi kubwa na kongwe zaidi nchini. Lakini ikiwa mashirika ya kibinadamu yapo tayari kusaidia, bajeti ni ngumu kutosheleza mambo muhimu yanayohitajika. Msaada wa chakula umepunguzwa, na kuathiri lishe.

Katika kituo cha afya cha 2 cha kambi ya wakimbizi ya Nakivale, kwenye kuta za majengo, kuna ujumbe wa kujilinda dhidi ya madhara ya utapiamlo. Hapa, ni katika kambi mnamo Machi 7, 2024.
Katika kituo cha afya cha 2 cha kambi ya wakimbizi ya Nakivale, kwenye kuta za majengo, kuna ujumbe wa kujilinda dhidi ya madhara ya utapiamlo. Hapa, ni katika kambi mnamo Machi 7, 2024. © Paulina Zidi / RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum katika Nakivale, Paulina Zidi

Katikati ya Nakivale, sekta ya Juru imeshuhudia wakimbizi wengi wapya wakipata makazi katika miezi ya hivi karibuni. Na kama wale ambao tayari wako kambini hapo kwa muda mrefu, Jean-Didier, Sébastien na Simon wanazungumza kauli moja : maisha ni magumu sana.

"Hatuna chochote cha kula," mmoja wao anasema. "Tupo hapa, lakini maisha ni magumu sana. Hatuna chakula kwa vile hatuna mashamba ya kulima,” anaongeza mwingine. “Unapokosa chakula, unapokosa maji, yote hayo, pia hukosa usalama kichwani. "

Jean-Didier ana wasiwasi skuhusu mke wake, ambaye ana mimba ya mtoto wake wa kwanza ambaye anatarajiwa kuzaliwa katika siku zijazo: katika kambi hii, vijana na wasichana ndio ambao wameathiriwa zaidi na utapiamlo, hasa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5. Kwa sasa, 40% ya wale wanaoishi Nakivale wana utapiamlo. Pamoja na athari kubwa juu ya maendeleo yao.

Wasiwasi ulioshirikiwa na Daktari Justin Okello, mkuu wa kituo cha afya: “Ubongo wa mwanadamu hukua sana katika siku 1,000 za kwanza za maisha. Na kila kitu kinachoenda vibaya kitakuwa na athari. Mtoto atakuwa na ugumu wa kuwa mwanafunzi mzuri, mtu mzima mwenye tija ambaye anachangia ukuaji. Kwa hiyo kutakuwa na madhara kwa jamii, kwa mtoto na familia yake.”

Kutokana na kuendelea kwa migogoro nchini Sudan na DRC, wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu huko Nakivale wanahofia kupunguza msaada wa chakula kwa mara nyingine tena.

Kutokana na uhaba huu wa misaada, baadhi ya watendaji wakuu wa masuala ya kibinadamu hata wamelazimika kufanya maamuzi makubwa na kurekebisha mbinu zao za usaidizi. Hivi ndivyo ilivyo kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) la Umoja wa Mataifa.

Mnamo mwaka wa 2023, kulingana na takwimu kutoka kwa wahusika, ni 35% tu ya mahitaji ya kibinadamu kwa wakimbizi nchini Uganda yamefadhiliwa: haiwezekani katika hali hizi kudumisha misaada yote ya chakula kwa watu wote wanaohusika, yaani milioni 1.6 nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.