Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA-IRAQ-ISIL-Usalama

Marekani: Baraza la wawakilishi laidhinisha mpango wa kuwasaidia waasi wa Syria

Jumatano jioni wiki hii Baraza la wawakilishi nchini Marekani, lenye wabunge wengi kutoka chama cha Republican limeipigia kura bajeti ihusuo kugharamia mazoezi ya kijeshi kwa waasi wa Syria wenye msimamo wa wastani. Bajeti hiyo imepasishwa kwa kura 273 dhidi ya 156.

Makao makuu ya Baraza la wawakilishi nchini MArekani, ambalo limeidhinisha mpango wa kuwasaidia kijeshi waasi wa Syria.
Makao makuu ya Baraza la wawakilishi nchini MArekani, ambalo limeidhinisha mpango wa kuwasaidia kijeshi waasi wa Syria. AFP/Mark Wilson
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye hahitaji kura kwa kuendesha mashambulizi nchini Iraq na Syria dhidi ya wapiganaji wa Islamic State, amekua akisubiri idhini ya Baraza la wawakilishi kwa kugharamia mashambulizi hayo na kuwasaidia kijeshi waasi wa Syria wenye msimamo wa wastani.

Mpango huo wa serikali ya Marekani hauhitaji wabunge wote kuupigia kura, lakini unapaswa kutekelezwa baada ya Baraza la wawakilishi kutoa idhni ya matumizi ya fedha kwa kugharamia mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State na kuwasaidia wapiganaji wa Syria wenye msimamo wa wastani dhidi ya utawala wa Bashar Al Assad. Ili bajeti hiyo iweze kupita moja kwa moja inabidi Baraza la Seneti litowe msimamo wake kwa kupiga kura ambayo , ambayo inatazamiwa kufanyika alhamisi au ijumaa wiki hii.

Wabunge kutoka chama cha Conservative katika Baraza la wawakilishi lenye wabunge wengi kutoka chama cha Republican wamepiga kura ya kuunga mkono mpango huo wa Barack Obama. Wabunge wengi kutoka chama cha Democrat wamepiga kura ya kupinga mpango huo wakielezea hofu yao kuona Marekani inajingiza katika machafuko ambayo yanaweza kuisababishia hasara kubwa.

Tawi la mrengo wa kushoto bado hawana imani na rais juu ya ahadi yake ya kutotuma wanajeshi wa ardhini kupambana wapiganaji wa Islamic State. Hivi karibuni raia wa Marekani walipiga kura ya kupinga Marekani kuendelea na vita katika mashariki ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.