Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-Usalama

Pyongyang na Seoul zanyoosheana kidole

Korea Kaskazini inaishtumu Korea Kusini kwa kulemaza kwa makusudi juhudi za upatikanaji wa amani ya kudumu kati ya nchi hizo jirani.

Hwang Pyong-so, ambaye anachukua nafasi ya pili katika utawala wa Korea Kaskazini, akiwa ziarani Korea Kusini, Oktoba 6 mwaka 2014.
Hwang Pyong-so, ambaye anachukua nafasi ya pili katika utawala wa Korea Kaskazini, akiwa ziarani Korea Kusini, Oktoba 6 mwaka 2014. Ed Jones/AFP
Matangazo ya kibiashara

Pyongyang inasema Seoul imeendelea kufanya mazoezi ya kijeshi hali ambayo imeendelea kuzua hali ya wasiwasi kati ya nchi hizo mbili.

Malalamishi haya ya Korea Kaskazini yanakuja wakati huu, nchi hizo mbili zikiafikiana kuanza mazungumzo ya pamoja yanayolengakumaliza wasiwasi wa kisualama miongoni mwao.

Hata hivyo viongozi wa kijeshi wa Korea hizo mbili walikutana kwa mara ya kwanza Jumatano wiki hii tangu miaka saba iliyopita.

Mazungumzo kati ya viongozi hao wa kijeshi yalifanyika katika kijiji cha Pan Munmunjeom, katika eneo la mpaka kati ya mataifa hayo mawili.

Pyongyang imeiomba Seoul kuachana na tabia ya kusambaza nyaraka zinazopiga vita utawala wake. Ijumaa wiki iliyopita majeshi ya nchi hizo yalishambuliana kwa silaha nzito, bila hata hivo kusababisha hasara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.