Pata taarifa kuu
CHINA-Maandamano-Siasa

Mgawanyiko wajitokeza kati ya waandamanaji Hong Kong

Mgawanyiko umejitokeza kati ya waandamanji juu ya mustakabali wa vuguvugu (Occupy Central) lililoanzishwa na wanafunzi wa vyuo vikuu kutaka kuwepo na mfumo wa demokrasia katika jimbo la Hong Kong.

Viogozi wa vuguvugu Occupy Central (kushoto-kulia) Benny Tai, Alex Chow, Joshua Wong, Alan Leong na Woo Mei Lin, wakishikana mikono, Oktoba 26 mwaka 2014. Wamehitilafiana kufuatia hatama ya vuguvugu lao.
Viogozi wa vuguvugu Occupy Central (kushoto-kulia) Benny Tai, Alex Chow, Joshua Wong, Alan Leong na Woo Mei Lin, wakishikana mikono, Oktoba 26 mwaka 2014. Wamehitilafiana kufuatia hatama ya vuguvugu lao. REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Vuguvugu hilo liko mbioni kusambaratika, baada ya waanzilishi wa Occupy Central kutoa wito kwa wanafunzi wanaounga mkono mfumo wa kidemokrasia kuondoka katika maeneo yaliyo karibu na makao makuu ya serikali. Wanafunzi hao wameonekana kufutilia mbali wito huo. Mamia ya mahema ya waandamanaji yemeendelea kuwepo katika barabara za mji wa Admiratly.

Awali yalikua makundi matatu. Kila kundi lilikua na jukumu la kuendesha harakati zake katika maandamano hayo yaliyodumu muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa, hususan kuhamasisha watu wengi zaidi kufikiri na kustahamili baridi, mvua pamoja na utumiaji nguvu wa polisi.

Lakini tangu waanzilishi watatu wa Occupy Central watangaze nia yao ya kujielekeza kwenye makao makuu ya polisi leo Jumatano Desemba 3, huku Joshua Wong, kiongozi wa vijana wa vuguvugu la Scholarism akitangaza nia yake ya kuendelea na mgomo wa njaa pamoja na kuendelea kushikilia baadhi ya maeneo, waandamanaji wameanza kuwa na mashaka.

Serikali ina njia mbili muhimu. Aidha ikubali, kama wanavyodai waandamanaji vijana kuanzisha mazungumzo juu ya mabadiliko ya kisiasa. Aidha ichukuliye kipindi hiki ambapo waandamanaji wamehitilafiana kutuma polisi kuwaondoa katia maeneo wanayoshikilia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.