Pata taarifa kuu
CHINA-RIADHA-MCHEZO

Sebastian Coe, rais mpya wa Shirikisho la kimataifa la Riadha

Bingwa wa zamani wa michezo ya Olimpiki katika riadha mbio za Mita 1500 Sebastian Coe raia wa Uingereza amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la riadha duniani IAAF.

Sebastian Coe, rais mpya wa IAAF, akifanya mkutano na waandishi wa habari  akiwa pamoja na mtangulizi wake Lamine Diack, Agosti 19 mwaka 2015, mjini Beijing.
Sebastian Coe, rais mpya wa IAAF, akifanya mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na mtangulizi wake Lamine Diack, Agosti 19 mwaka 2015, mjini Beijing. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Coe alipata kura 115 na kumshinda mpinzani wake Sergey Bubka raia wa Ukraine aliyepata kura 92 wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumatano wiki hii njini Beijing.

Sebastian Coe, bingwa mara mbili wa mchezo wa Olimpiki katika mbio za mita 1500 katika miaka ya (1980/1984), anachukua na fasi ya Lamine Diack, raia wa Senegal, mwenye umri wa miaka 82, ambaye alikua kwenye uongozi wa shirikisho hilo kwa kipindi cha mika 15 na miezi tisa.

Raia huyo wa Uingereza sasa atachukua uongozi wa riadha duniani mwisho wa mwezi huu baada ya kumalizika kwa mashindano ya dunia ya riadha na atachukua nafasi ya Lamine Diack raia wa Senegal anayestaafu baada ya kuongoza Shirikisho hilo tangu mwaka 1999.

Kiongozi huyu mpya anatarajiwa kuwa madarakani kwa miaka minne akiwa na kazi kubwa ya kukabiliana na tuhma za idadi kubwa ya wanariadha kutumia dawa za kusisimua misuli ili kushinda medali.

Coe amesema atapendekeza kuundwa kwa tume ya kujitegemea kuchunguza madai ya wanariadha wanaotumia dawa hizo.

Uchaguzi huu umefanyika siku mbili kabla ya kuanza kwa mashindano ya riadha ya dunia jijini Beijing.

Mtangulizi wake, Lamine Diack, raia wa Senegal, anaondoka kwenye wadhifa wake baada ya kufanya kazi kubwa ya kulitengeneza shirikisho hilo kuwa la kimataifa, lakini linakabiliwa na utata juu ya madawa ya kulevya.

Ni ukurasa katika historia ya mchezo wa Kiafrika na ulimwenguni ambao unageuza taswira Jumatano Agosti 19 mwaka 2015. Lamine Diack, mtu wa kwanza barani Afrika kuongoza shirikisho kubwa la kimataifa la mchezo wa Riadha ameondoka kwenye wadhifa huo Agosti 19 mwaka 2015 mjini Beijing. Lamine Diack, alichaguliwa kuliongoza shirikisho la kimataifa la mchezo wa Riadha mwaka 1999.

Katika uongozi wake, Lamine Diack hakufurahia mashindano ya dunia ya Riadha yafanyike barani Afrika. Hata hivyo, raia huyo wa Senegal alijikita sana na bara la Asia. Chini ya uongozi wake, mashindano ya Dunia ya mchezo huu yalifanyika katika mji wa Osaka, Japan ( mwaka 2007), katika mji wa Daegu, Korea Kusini ( mwaka 2011), katika mji wa Beijing, nchini China ( mwaka 2015). Lamine Diack, Meya wa zamani wa mji wa Dakar pia alihudhuria katika uteuzi wa Doha (Qatar) kuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya Raidha ya mwaka 2009.

Shirikisho la kimataifa la Riadha liliundwa mwaka 1912 (IAAF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.