Pata taarifa kuu
YEMENI-MAZUNGUMZO-USALAMA-SIASA

Yemen: mazungumzo ya amani kuanza Desemba 15

Mazungumzo ya amani chini ya usuluhishi wa Umoja wa Mataifa yataanza Desemba 15 nchini Uswisi ili kujaribu kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vimesababidha vifo vya watu 6,000 nchini Yemen.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ismail Ould Cheikh Ahmed, atoa wito kwa zote husika kusitisha mapigano kuanzia Desemba 15.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ismail Ould Cheikh Ahmed, atoa wito kwa zote husika kusitisha mapigano kuanzia Desemba 15. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Ismail Ould Cheikh Ahmed, ambaye ametoa tangazo hilo Jumatatu hii , amezitaka pande zote katika vita vinavyoendelea kusitisha mapigano kuanzia tarehe hiyo.

Serikali ya Rais Abd-Rabbou Mansour Hadi ilio uhamishoni na waasi wa Kishia wa Huthi wanaoungwa mkono na Iran wanashiriki katika mchakato wa amani ulioanzishwa katika majira ya joto mwaka huu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ismail Ould Cheikh Ahmed ameongeza.

Azimio 2216, lililopitishwa Aprili 14, linazitaka pande husika katika vita nchini Yemen kukomesha matumizi ya nguvu na kujiepusha na hatua yoyote ambayo inaweza kuhatarisha mchakato wa mpito wa kisiasa. Azimio hilo pia linawataka wanamgambo wa huthi kuondoka kutoka maeneo yote walioyateka tangu mgogoro kuanza mwezi Septemba mwaka 2014, "ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Sanaa."

Vikosi vinavyomuunga mkono Rais Hadi, tangu mwishoni mwa mwezi Machi na muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia, wanashiriki kwa miezi tisa sasa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi waasi wa Huthi.

Wanamgambo wa Huthi kwa sasa wanaudhibiti mji wa Taiz, kaskazini mwa Aden.

"Nimezisihi pande zinazohusika katika vita vinavyoendelea nchini Yemen kushirikiana katika hatua za kujenga imani, ikiwa ni pamoja na kukomesha mapigano, kuwaachilia huru wafungwa na kuweza kutoa na fasi ili misaada ya kibinadamu iwafikie walengwa", Ould Cheikh Ahmed amesema mjini Geneva, ambako amethibitisha ufunguzi wa mazungumzo hayo katika eneo ambalo linasalia kutajwa.

"Ni matumaini yetu ya kupata mkataba wa kusitisha mapigano ambao utaanza kutekelezwa mwanzoni mwa mazungumzo lakini katika hali ya kuimarisha na kuhakikisha kwamba mkataba huo unadumu na kusitisha moja kwa moja mapigano", mwanadiplomasia huyo kutoka Mauritania ameongeza.

Awali Ould Cheikh Ahmed alipokelewa na rais Hadi katika mji wa Aden na viongozi wa wanamgambo wa Kishia wa Houthis katika mji wa Muscat, mji mkuu wa Oman, ambapo aliwasilisha rasimu ya ajenda ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.