Pata taarifa kuu
BANGLADESH-USALAMA

Bangladesh: Saba wauawa kwa kupigwa risasi katika kambi ya wakimbizi ya Rohingya

Washambuliaji wamewauwa watu wasiopungua saba Ijumaa katika shambulio kwenye seminari ya Kiislamu katika kambi ya wakimbizi ya Rohingya nchini Bangladesh, mpakani na Burma, polisi wamesema.

Kambi ya wakimbizi ya Rohingya ya Kutupalong, Bangladesh, Novemba 23, 2017.
Kambi ya wakimbizi ya Rohingya ya Kutupalong, Bangladesh, Novemba 23, 2017. Marcus Valance/SOPA Images/LightRocket via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wahanga waliuawa kwa kupigwa risasi, wengine walidungwa visu, mkuu wa polisi wa eneo hilo almeliambia shirika la habari la AFP.

Mauaji hayo yanajiri wakati mivutano ikiongezeka baada ya mauaji ya kiongozi wa Rohingya katika kambi moja wiki tatu zilizopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.