Pata taarifa kuu

Japani: Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi yaongezeka hadi 62

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Japani katikati mwa Japani siku ya Jumatatu, Siku ya Mwaka Mpya, imeongezeka hadi vifo 62 kulingana na hesabu mpya iliyofanywa Jumatano na mamlaka katika eneo hilo.

Jengo lililoporomoka, ahli iliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililopiga Wajima, katika mkoa wa Ishikawa, Japani Januari 2, 2024.
Jengo lililoporomoka, ahli iliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililopiga Wajima, katika mkoa wa Ishikawa, Japani Januari 2, 2024. via REUTERS - KYODO
Matangazo ya kibiashara

Afisa kutoka idara ya Ishikawa, aliyehojiwa na shirika lahabari la AFP lakini ambaye hakutaka kutaja jina lake, amezungumzia "vifo 62" na kutaja zaidi ya majeruhi 300, ikiwa ni pamoja na 20 ambao wako katika hali mbaya.

Serikali imefungua njia ya bahari kupeleka misaada na baadhi malori makubwa sasa yanaweza kufikia katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi.

Barabara zimeharibika vibaya, miundombinu imebomoka, na maeneo ya mbali ambayo yameathirika vibaya imekuwa vigumu kufikika na kufanikisha juhudi za uokozi. Hadi wakati huu taarifa kamili za athari zilizotokea bado hazijaweza kufahamika ikiwa ni takribani siku mbili baada ya kutokea balaa hilo.

Jumatatu alasir tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha 7.6 lilipiga eno la Noto, kuzisambaratisha nyumba na kusababisha ugumu wa kufikisha misaada ya kiutu yenye kuhitajika sana katika maeneo ya mbali ya taifa hilo.

Mvua kubwa imetabiriwa katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo Jumatano hii na hivyo kuongeza hofu ya maporomoko ya ardhi. Taarifa hiyo imezusha hofu kwa juhudi za serikali katika kuwanusuru watu wengi ambao wamenasa kwenye vifusi.

Mwaka 2011, Japan ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la ukubwa wa 9.0 katika kipimo cha Richter,  ambalo lilisababisha tsunami iliyosababisha vifo vya takriban watu 18,500 huko upande wa kaskazini/mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.