Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa wabunge Bangladesh: Waziri Mkuu Sheikh Hasina apata ushindi usio wa kawaida

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina anaelekea muhula wa tano - wa nne mfululizo - baada ya kushinda uchaguzi wa wabunge Jumapili hii, Januari 7, uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani ambacho kilishutumu "uchaguzi wa udanganyifu".

Akiwa madarakani tangu 2009, Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina anaelekea muhula wa nne mfululizo. Dhaka, Januari 7, 2024.
Akiwa madarakani tangu 2009, Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina anaelekea muhula wa nne mfululizo. Dhaka, Januari 7, 2024. AP - Mahmud Hossain Opu
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Ligi Awami "kimeshinda zaidi ya 50% ya viti" katika Bunge, msemaji wa tume ya uchaguzi ameliambia shirika la habari la AFP, saa chache baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa. Muda mfupi kabla, Somoy TV, kituo kikubwa zaidi cha televisheni cha kibinafsi katika nchi hii yenye wakazi milioni 170, kimetangaza kuwa Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Sheikh Hasina amehakikishiwa ushindi, chama chake kikiwa na washirika wake kushinda angalau 60% ya viti vya Bunge, baada ya kutangazwa ya matokeo ya viti 225 kati ya 300.

Baada ya kupiga kura huko Dhaka, Sheikh Hasina, 76, alitoa wito kwa wapiga kura kupiga kura, akiahidi uchaguzi "huru na wa haki". Pia alikishutumu chama kikuu cha upinzani, Bangladesh Nationalist Party (BNP) kwa kususia uchaguzi, akikitaja kama "kundi la kigaidi".

BNP, kwa upande wake, imeshutumu "uchaguzi wa udanganyifu". Uchaguzi huo pia umesusiwa na vyama vingine. Chama cha Ligi ya Awami hakikuwa na wapinzani katika maeneo ambayo kiligombea. Lakini kiishindwa kuwasilisha wagombea katika baadhi ya maeneo, ikionekana kukwepa Bunge kuonekana kama chombo cha chama kimoja.

Mkuu wa tume ya kitaifa ya uchaguzi alikadiria ushiriki wakati wa mchana kwa karibu 40%. Wananchi wengi wa Bangladesh waliohojiwa na shirika la habari la AFP walisema hawakupiga kura kwa sababu matokeo yalikuwa hitimisho lililotarajiwa. Kiongozi wa chama cha BNP, Tarique Rahman, aliye uhamishoni, alikashifu uwezekano wa ujazo wa kura. Ushuhuda mwingi uliripoti motisha mbalimbali, hata usaliti, kutoka kwa mamlaka ili kuhimiza ushiriki. Baadhi ya wapiga kura wanasema walitishiwa kunyang'anywa kadi zao za manufaa za serikali, muhimu ili kupata manufaa ya kijamii, ikiwa watakataa kupigia kura chama cha Awami League.

Siku ya uchaguzi yenye wasiwasi

Chaguzi hizi za wabunge zilifanyika katika hali ya wasiwasi. Takriban maafisa wa polisi 700,000 na askari wa akiba, na karibu wanajeshi 100,000, walitumwa kudumisha utulivu wakati wa upigaji kura, kulingana na tume ya uchaguzi. Mashariki mwa nchi, huko Chittagong, polisi walifyatua risasi, bila kusababisha majeraha yoyote, kuwatawanya karibu wanaharakati sitini wa upinzani ambao walikuwa wameweka kizuizi cha barabarani kupinga uchaguzi huo, kulingana na polisi wa eneo hilo.

BNP na vyama vingine viliandamana bila mafanikio kwa miezi kadhaa mwishoni mwa mwaka 2023 kushinikiza kujiuzulu kwa Seikh Hasina na serikali isiyoegemea upande wowote kusimamia uchaguzi. Baadhi ya viongozi wa upinzani 25,000, ikiwa ni pamoja na viongozi wote wa ndani wa chama cha BNP, walikamatwa baada ya maandamano haya, ambapo watu kadhaa waliuawa katika makabliano na polisi, kulingana na chama hicho. Serikali, kwa upande wake, iliripoti kukamatwa kwa watu 11,000.

Tangu arejee madarakani mwaka 2009, Sheikh Hasina ameimarisha udhibiti wake baada ya chaguzi mbili zilizokumbwa na kasoro na tuhuma za udanganyifu. Ingawa serikali yake inashutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na kutekeleza ukandamizaji wa kikatili dhidi ya upinzani, mafanikio yake ya kiuchumi kwa muda mrefu yameunga mkono umaarufu wake. Lakini matatizo yameongezeka hivi karibuni, na kupanda kwa bei na kuenea kwa tatizo la kukatika kwa umeme. Muhula wake wa tano, wa nne mfululizo, kwa hivyo unaonekana kuwa dhaifu.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.