Pata taarifa kuu

Marekani: Uchaguzi wa Bangladesh 'haukuwa huru wala wa haki'

Diplomasia ya Marekani inakooa mazingira ya uchaguzi nchini Bangladesh, ambapo Waziri Mkuu Sheikh Hasina alishinda, lakini ukisusiwa na upinzani na baadhi ya watu wanazuliwa. 

Bango la uchaguzi unaotoa nafasi kubwa ya kushinda kwa Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina mnamo Januari 3, 2024 huko Dhaka.
Bango la uchaguzi unaotoa nafasi kubwa ya kushinda kwa Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina mnamo Januari 3, 2024 huko Dhaka. © Mohammad Ponir Hossain / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Marekani inashiriki msimamo wa waangalizi wengine kwamba uchaguzi huu haukuwa huru wala wa haki, na tunasikitika kwamba vyama vyote havikuweza kushiriki," msemaji wa Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani  Matthew Miller, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu.

Chama cha Ligi Awami "kimeshinda zaidi ya 50% ya viti" katika Bunge, msemaji wa tume ya uchaguzi aliliambia shirika la habari la AFP, saa chache baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa. Muda mfupi kabla, Somoy TV, kituo kikubwa zaidi cha televisheni cha kibinafsi katika nchi hii yenye wakazi milioni 170, kilitangaza kuwa Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Sheikh Hasina amehakikishiwa ushindi, chama chake kikiwa na washirika wake kushinda angalau 60% ya viti vya Bunge, baada ya kutangazwa ya matokeo ya viti 225 kati ya 300.

Baada ya kupiga kura huko Dhaka, Sheikh Hasina, 76, alitoa wito kwa wapiga kura kupiga kura, akiahidi uchaguzi "huru na wa haki". Pia alikishutumu chama kikuu cha upinzani, Bangladesh Nationalist Party (BNP) kwa kususia uchaguzi, akikitaja kama "kundi la kigaidi".

BNP, kwa upande wake, ilishutumu "uchaguzi wa udanganyifu". Uchaguzi huo pia ulisusiwa na vyama vingine. Chama cha Ligi ya Awami hakikuwa na wapinzani katika maeneo ambayo kiligombea. Lakini kiishindwa kuwasilisha wagombea katika baadhi ya maeneo, ikionekana kukwepa Bunge kuonekana kama chombo cha chama kimoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.