Pata taarifa kuu
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO-Mapigano

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR watoroka kituo chao muhimu baada ya kushambuliwa na jeshi la DRCongo

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR waliopiga kambi mashariki mwa DRCongo wamearifiwa kutoroka kituo chao muhimu baada ya shambulio lililoendeshwa na majeshi ya serikali yakisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa huku wakiacha vifaa vyao katika uwanja wa mapambano.

Vifaru vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Vifaru vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Serikali ya DRCongo FARDC likisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa UN kutoka nchini India walishambulia kituo cha wapiganaji hao wa Kihutu katika eneo la Kalengera kwenye umbali wa kilomita zaidi ya hamsini na jiji la Goma.

Makundi mengi ya waasi, mkiwemo kundi hili la FDLR, yamekua yakiendesha shughuli zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hasa katika mkoa wa Kaivu kasakazini.

Baadhi ya viongozi wa kundi la FDLR wanatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani, yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Kwa mujibu wa maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Congo, makabiliano ya jumapili yalipelekea kundi la FDLR kupoteza wapiganaji wake wawili na wengine watano kujeruhiwa, lakini hakuna hasara iliyotokea upande wa jeshi.

Mapigano yamedumu “saa moja”, amesema mmoja kati ya maafisa hao, huku akibaini kwamba mamia ya wapiganaji wa FDLR wamekua wakitumia bunduki aina ya kalachnikovs na silaha nzitonzito, lakini sehemu kubwa ya wapiganaji hao wamekimbilia katika hifadhi ya wanyama ya Virunga.

Umoja wa Mataifa umewatolea wito wapiganaji hao wa Kihutu kutoka Rwanda kujisalimisha kwa hiari na kuweka silaha chini kabla ya kunyang'anywa kwa nguvu katika operesheni ya kijeshi ya Umoja huo na vikosi vya serikali.

Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Monusco Martin kobler amewataka wapiganaji hao kujisalimisha haraka iwezekanavyo na kuachana na viongozi wao ambao wanakabiliwa na kesi ya kujibu mbele ya mahakama.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.