Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC-Usalama

Burundi: zoezi la kuwaondoa wanajeshi Congo

Wiki hii kumekuwa na taarifa ya kuanza kwa zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa Burundi katika eneo la Kiliba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya viongozi wa mataifa ya Burundi na Congo kujizuia kutoa taarifa yoyote kuhusu zoezi hilo.

Kanali Gaspard Baratuza, msemaji wa jeshi la Burundi.
Kanali Gaspard Baratuza, msemaji wa jeshi la Burundi. Burunditransparence.org
Matangazo ya kibiashara

Awali serikali ya Burundi na Congo zilikanusha kuwepo kwa wanajeshi wa Burundi katika aridhi ya Congo, baada ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Congo Monusco kuthibitisha kuwepo kwa wanajeshi hao.

Wakaazi wa eneo la Gatumba nchini Burundi wamesema wameona gari la afisa wa Idara ya Ujasusi ajulikanaye kwa jina la Kazungu, likibeba vitu vizito wakishuku kwamba huenda ni silaha.

Kwa upande wake mkuu wa kundi la vijana wa chama tawala Cndd-Fdd “ Imbonerakure”, Denis Karera, amekanusha kuonekana kwa gari lake kwenye eneo jeshi la Burundi liliyokua likipiga kambia mashariki mwa Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.