Changu Chako, Chako Changu
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Utamaduni wa kupenda kujifunza lugha na msanii kutoka Burundi Mistachampagne
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na vijana wanafunzi na waalimu wa lugha ya kifaransa kuangazia utamaduni wa kujifunza lugha hususan lugha ya Kifaransa, wakati kwenye kipengele cha Muziki amempokea mwanamuziki kutoka nchini Burundi Mistachampagne ambae anazuri jiji la Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.28/01/202420:04 -
Kumbukumbu ya Makala za mwaka 2023 alizokukusanyia Ali Bilali
Makala haya ni mkusanyko wa Makala za mwaka 2023 alizokukusanyia mtangazaji wako Ali Bilali27/01/202420:02 -
Historia ya kabila la Wadigo wa Kenya na Tanzania katika Makala Changu Chako na Florence Kiwuwa
Katika Makala haya,Florence Kiwuwa mtangazaji wa maswala ya Historia na utamaduni kutoka RFI Kiswahili anakuletea historia ya wadigo wa Kenya na Tanzania na kwenye le Parler francophone tutaangazia kuhusu maonyesho yake Dj Click katika ukumbi wa Alliance Francaise ya Arusha nchini Tanzania. Na kwenye Muziki tutamuangazia mwanamuziki Koffi Olomide kutokea DRC.28/11/202320:03 -
Tamaduni za watu wa Katanga katika uchimbaji wa madini na msanii Masauti kutoka nchini Kenya
Ni furaha kubwa kukutana nawe kwa mara nyingine tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu ambapo leo nitaungana na mwenzangu DENISE MAYO kukujuza kuhusu tamaduni za watu wa huko Katanga katika uchimbaji wa madini, kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba wa Alliance francaise za Ukanda na Institut Français ya Lubumbashi, kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Kutoka nchini Kenya Mohammed Ali Said, anaefahamika sana kama Masauti. Mimi ni Ali Bilali19/11/202319:59 -
Utamaduni wa kabila la Wataita na mwanamuziki Hiro le Coq katika Makala haya ya leo.
Karibu mpenzi msikilizaji katika Makala ya leo Changu Chako Chako Changu, ambapo nakukumbusha historia na tamaduni ya watu wa kabila la wataita, na kwenye le parler francophone tutaangazia ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance France Francaise ya Nairobi, Dar es salaam, Arusha, na Institut francais ya Lubumbashi. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Hiro Le Coq rapa wa Ufaransa mwenye asili ya DRC. Mimi naitwa Ali Bilali bienvenue.13/11/202319:56 -
Mwanahabari kutoka DRC ashinda Toleo ka kumi la tuzo Ghislaine Dupont na Claude Verlon
Makala haya yanazungumzia kuhusu tolea la 10 la tuzo ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon ambalo hutolewa kila Novemba 02 ya kila mwaka na RFI ili kuwaenzi waandishi wa habari hao wawili waliofariki miaka 10 iliopita huko Kidal kaskazini mwa Mali baada ya kutekwa na wanajihadi, ambapo Joseph Kahongo wa (RDC) na Ange J. Agbla (Bénin) ndie washindi wa toleo hili la kumi. ambatana naye Ali Bilali kudahamu mengi zaidi.09/11/202319:57 -
Historia ya siku ya kupinga dhulma dhidi ya wanahabari na utoaji wa tuzo ya Ghislaine Dupont
Leo Octoba 29 kwenye Makala Changu chako Chako Changu tunazungumzia kuhusu historia ya Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Kutokujali kwa Uhalifu Uliotendwa dhidi ya Wanahabari ambayo huadhimishwa kila Novemba 2. Na kwenye le parler francophone kama kawaida nitakujuza nini kinachojiri kwenye vituo vya Alliance francaise ya Nairobi, Dar es Salaam na Arusha, na kwenye Muziki ninakuletea mwanamuziki Jay Melody kutoka nchini Tanzania. Bienvenue et Bon Dimanche, yaani Karibu na Jumapili njema.31/10/202319:53 -
Siku ya kimataifa ya utamaduni nchini Kenya Octoba 10
Karibu msikilizaji katika makala haya changu chako chako changu Jumapili ya leo ambapo Jumapili ya leo tunazungumzia kuhusu siku ya kitaifa ya utamaduni nchini Kenya ambayo huadhimishwa kila Octoba 10. Na kwenye le parler francophone tutaangazia namna shughuli za kitamaduni zinavyo pamba moto kuelekea mwisho wa mwaka Alliance Francaise ya Arusha, Nairobi na Dar es salaam na kwenye Muziki nitaungana na mwenzangu Benson Waokoli kuzungumzia kumbukumbu ya kifo cha francois Lwambo Lwanzo Maki16/10/202319:59 -
Hofu ya wananchi kuzuru Jumba la Makumbusho ya Kolwezi kisa uwepo wa mizimu
Ni furaha kubwa kukutana nawe kwa mara nyingine tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu ambapo leo naungana na mwenzangu Denise Maheho kukujuza kuhusu jumba la makumbusho la huko Kolwezi, na kwenye le parler francophone nitakujuza kuhusu shughuli za utamaduni kwenye vituo vya Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam na kwenye Muzki nitakuletea mwanamuziki Diamond Plantnumz ambae juma hili ameadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.09/10/202319:59 -
Abu Omar mwanamuziki wa zamani wa muziki wa Densi atambulisha kitabu chake
Ni furaha kukutana nawe kwa mara nyingine tena Jumapili hii katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo leo nakuletea Msanii wa kitambo wa bendi kutoka Afrika mashariki Abu Omar ambae ameandika kitabu kuzungumzia historia ya muziki wa densi. Kwenye le parler francophone nakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance francaise ya Nairobi, na Dar es salaam, na kwenye muziki nakuletea muziki wa Singeli kutoka nchini Tanzania. Mimi ni mtangazaji asiependa makuu Ali Bilali. Binevenue.01/10/202320:00 -
Mambo mbalimbali katika tamaduni za watu wa Burundi na wa Kenya
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anakuletea tofauti mbalimbali za tamaduni za watu kutoka nchinbi Burundi na Kenya.23/09/202320:00 -
Historia ya waswahili wa Burundi sehemu ya tatu ndani ya Changu Chako Chako Changu
Katika sehehemu hii ya tatu na ya mwisho ya makala kuhusu historia ya waswahili wa Burundi, mzee anzuruni anatueleza hapa kuhusu harakati za kumtambua mswahili wa Burundi zilipofikia. Utafahamu pia kuhusu historia ya mwanamuziki Jux kutoka nchini Tanzania. ambatana naye Ali Bllali hapa rfi kiswahili. usikosi pia kumfollow kwa instagram @billy_bilali10/09/202320:02 -
Sehemu ya pili ya makala Changu Chako Chako Changu kuhusu historia ya Waswahili wa Burundi
Ni furaha kubwa kukutana nawe Jumapili nyingine katikza Makala haya changu chako chako changu ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu historia ya waswahili wa Burundi. Na kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba ya shughuli kwenye Alliance francaise ya Nairobi, Dar es salaam na Alliance francaise ya Lubumbashi. Kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki kutoka nchini Burundi anaitwa Miraculos Lop. Mimi naitwa Ali Bilali mtangazji wako asiependa makuu. Bienvenue, ama Karibu04/09/202319:58 -
Historia ya waswahili wa Burundi katika Makala Changu Chako Chako Changu na Ali Bilali
Katika Makala haya, Ali Bilali mtangazaji wa maswala ya Historia na utamaduni kutoka RFI Kiswahili anakuletea historia ya waswahili wa Burundi katika mazungumzo na mzee mkongwe mwana Historia kutoka Buyenzi, Mzee Anzuruni Hussein, ikiwa ni sehemu ya kwanza, na kwenye le Parler francophone tutaangazia kuhusu ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamuangazia mwanamuziki Vichou Love kutoka nchini Burundi.27/08/202320:01 -
Wapemba wa Kenya wapewa vitambulisho vya uraia baada ya kutambuliwa
Ni furaha kubwa kwangu kukutana nawe kwa mara nyingine tena Jumapili ya leo katika Makala changu Chako Chako Changu, ambapo hivi karibuni rais wa Kenya aliwapa vitambulisho watu kutoka kabila la wapemba miezi kadhaa baada ya kuwaidhinisha kuwa miongoni mwa makabila ya wakenya, na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba ya shughuli kwenye Alliance francaise na Nairobi na Institut francais ya Lubumbashi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Ferre Golla Mimi ni Ali Bilali23/08/202319:51
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.