Changu Chako, Chako Changu
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Makala kuhusu Tamasha la MOCA lililofanyika huko Kigali Rwanda
Karibu kuwa nami Jumapili hii katika Makala Changu Chako Chako Changu, makala maalum kuhusu Tamasha lijulikanalo kama MOCA, Movement Of Creative Africas, yaani jukwaa la Viwanda vya Utamaduni na Ubunifu vya Kiafrika (ICC) na diaspora. Jumapili hii siko pekeangu nitakuwa naye mtangazaji mwenzangu ambae tumeambatana pamoja mpaka Kigali nchini Rwanda Florence Kihuwa.07/07/202219:50 -
Historia ya utawala wa ufalme wa Ubelgiji nchini DRCongo
Ni Jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya ya Changu Chako Chako Changu, ambapo leo nakuletea Historia ya Utawala wa Ufalme wa Ubelgiji nchini DRC, na kwenye Muziki nitakuletea historia ya mwanamuziki Ferre Gola ambae anakabiliwa na kesi huko nchini Ufaransa.21/06/202220:04 -
Utamaduni wa watu wa Afrika mashariki katika mambo mbalimbali
Katika Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amewapikea Studio Gez Gez Kasesa kutoka nchini Burundi na Dokta Gharib Mosepe kuzungumzia utamaduni wa watu kutoka Burundi na Kenya katika maswala mbalimbali. na kwenye Kipengele cha Muziki utapata kumfahamu mwanamuziki hayati Oliver Ngoma.15/06/202219:59 -
Historia ya jiji la Kisumu magharibu mwa Kenya sehemu ya pili
Karibu kuungana nami jumapili nyingine katika Makla haya ya Changu chako Chako changu rfi kiswahili leo nakuletea sehemu ya pili na ya mwisho kuhusu hitoria ya jiji la Kisumu, nitaungana naye mwenzangu Victor Abuso aliekuwepo huko Kisumu na kwenye kipengele cha le parler Francophone nitakuletea sehemu ya ratibu ya shughuli za kitamaduni kwenye Alliance Francaise ya Nairobi pamoja na Muziki nitakuletea mwanamuziki Anjella kutoka nchini Tanzania alie chini ya Lebo ya Konde Music Worldwide.04/06/202220:01 -
Historia ya jiji la Kisumu magharibi mwa Kenya
Ni Jumapili nyingine tunakutana tena katika Makla haya ya Changu chako Chako changu rfi kiswahili leo nakuletea hitoria ya jiji la Kisumu, nitaungana naye mwenzangu Victor Abuso aliekuwepo huko Kisumu na kwenye kipengele cha Muziki nitakuletea mwanamuziki muasisi wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania Mr Sugu mimi ni Ali Bilali bienvenue.28/05/202220:03 -
Sehemu ya mwisho kuhusu mjadala juu ya uchoraji vibonzo
sikiliza sehemu hii ya mwisho ya mjadala kuhusu uchoraji vibonzo pamoja na Muziki wa Dadju kutoka nchini Ufaransa.25/05/202220:18 -
Mjadala kuhusu uchoraji vibonzo baada ya tamasha la jijini Nairobi
Karibu kuwa nami kwa mara nyingine tena Jumapili hii katika Makla haya ya Changu Chako Chako Changu, ambapo leo nakuletea muendelezo wa Makala kuhusu uchoraji vibonzo na kwenye muziki nitamzungumzia hayati Robert Nesta Marley maharufu Bob Marley aliefariki miaka 41 iliopita.17/05/202220:01 -
Tamasha la Cartoons for peace and democracy na ujio mpya wa Wenge Musica BCBG 4X4
Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu chako Chako changu, ambapo leo nitakuletea kwa kiasi kikubwa maonyesho ya picha za katuni zilizchorwa na wasanii kutoka maeneo mbalimbali duniani, katika tamasha la Cartoons for Peace and Democracy, lakini pia nitakuletea kuungana tena kwa bendi ya wenge Musica BCBG 4X4 Tout terrain. Naitwa Ali Bilali. Bienvenue. Ama Karibu.07/05/202219:59 -
Historia ya siku kuu ya wafanyakazi duniani inayoadhimishwa Mai Mosi
Makala haya Changu Chako Chako Changu hii leo Ali Bilali anakuletea historia ya siku kuu ya Kimataifa ya wafanyakazi duniani, le parler francophone tutazungumzia kuhusu tamasha la vibonzo lililoandaliwa na ubalizi wa Ufaransa jijini Nairobi na kwenye muziki nitakuletea Muziki wa Papa Wemba lakini pia hatuwa ya serikali ya DRC kununua makaazi yake ya kifahari huko Kinshasa.02/05/202220:01 -
Utamaduni wa michango ya pesa kwenye sherehe za harusi
Katika Makala haya tunazungumzia kuhusu sherehe za harusi, le parler francophone na kwenye muziki nakuletea mwanamuziki kutoka Burundi anaitwa Vichou Love. Usikosi kuambatana nasi na unanafasi ya kutoa maoni au mapendekezo.26/04/202220:02 -
Safari ya mpiga picha Evans kutoka nchini Kenya
Makala haya yanamzungumzia mpiga picha Evans kutoka nchini Kenya na kwenye kipengele cha Muziki yanakuletea mwanamuziki kutoka katika kisiwa cha Mayotte anaitwa Zily20/04/202220:00 -
Historia ya kumbukumbu ya mauaji ya kimabri ya mwaka 1994 nchini Rwanda
Katika makala haya Changu Chako Chako Changu, leo nimekuandalia historia ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, le Parler Francophone na mwanamuziki Corneille mwenye asili ya Rwanda ambae amekuja na album yake mpya baada ya ukimya wa miaka takriban 10.Miaka 28 Tangu kutokea kwa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda, dunia imejifunza nini? Ukizingatia vurugu za jamhuri ya Afrika ya kati, mauaji ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwengineko.12/04/202220:01 -
Warsha ya kimataifa ya idhaa za kiswahili iliofanyika mjini Arusha nchini Tanzania
Katika Makala haya utapata kufahamu zaidi kuhusu warsha ya kimataifa ya idhaa za kiswahili iliofanyika mjini Arusha na kujumuisha vituo mbalimbali vya idhaa za kiswahili kutoka ukanda wa Afrika mashariki.07/04/202220:00 -
Mauaji yaendelea DRC mbele ya kimya cha jumuia ya kimataifa, Vaudou danse ya Benin
Makala hii imeangazia filamu yenye maudhui kuhusu mapigano na mauaji ya raia katika nchi ya DRC lakini pia sehemu ya pili ya mahojiano na mwalimu wa fazihi za Ufaransa, mtunzi na mwalimu. Katika kipengee cha muziki utawasikiliza wanamuziki wa bendi lifahamikalo kama BIM, Benin International Musical pamoja na mambo mengineUngana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka katika makala hii.19/03/202219:52 -
Mazungumzo maalum na Alain Mabanckou
Kwa kiasi kikubwa, tunamwangazia mwandishi wa vitabu, mwanahabari na mtunzi wa fasihi kifaransa pia msomi Alain Mabanckou, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Congo Brazaville.Yupo jijini Nairobi nchini Kenya kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya Francophonie.13/03/202219:56
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.