Pata taarifa kuu
SYRIA-KOBANE-EU-Usalama

Jamii ya Wakurdi wa Ulaya yaendelea kuunga mkono ndugu zao wa Syria

Mapigano yameendelea kurindima katika mji wa Kobane kati ya wapiganaji wa Dola la kiislam na wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria.  

Raia 160 000 wa Syria wahayama makaazi yao mjini Kobane wakikimbilia Uturuki.
Raia 160 000 wa Syria wahayama makaazi yao mjini Kobane wakikimbilia Uturuki. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Wakati wapiganaji wa dola la Kiislam wakiendelea na harakati zao za kuudhibiti mji wa Wakurdi wa Kobane, baada ya kuyadhibiti baadhi ya maeneo ya mji huo na vitongoji vyake, jamii ya wakurdi wa Ulaya wamekua wakihamasishana kwa minajili ya kuunga mkono ndugu zao wa Syria.

Watu hao kutoka jamii ya Wakurdi waishio barani Ulaya, wameandamana Jumanne wiki hii katika mataifa mengi ya Ulaya, wakidai kwamba ndugu zao wa Syria wanakabiliwa na vitisho vya kuuawa vinavyofanywa na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Mamia ya waandamanaji hao wamefaulu jana Jumanne kuingia katika jengo la Bunge la Ulaya, mjini Brussels, nchini Ubelgiji. Wakivalia nguo zenye picha ya Abdullah Ocalan, kiongozi wa chama cha kikurdi cha PKK (kiliyoanzishwa nchini Uturuki), walipenya na kufaulu kuingia katika jengo hilo, huku baadhi ya wabunge wa Ulaya wakiwaunga mkono.

Siku moja kabla, zaidi ya watu sitini kutoka jamii ya Wakurdi nchini Uholanzi waliandamana kwa utulivu dhidi ya kile wanachodai “ vitisho vya mauaji ya halaiki vinavyoandaliwa na wapiganaji wa Dola la Kiislam katika mji wa Kobane”, mji ambao ni watatu unaokaliwa na watu kutoka jamii ya Wakurdi, nchini Syria.

Jumatatu pia, mamia ya Wakurdi walikusanyika mbele ya Uwanja wa ndege wa Roissy-Charles-de-Gaulle, nchini Ufaransa, wakitolea wito serikali ya Ufaransa kulani tabia za baadhi ya raia wa mataifa ya Ulaya ambao wamekua wakisafiri nje ya bara hilo na kujiunga na makundi ya kijihadi, wakipitia kwenye viwanja vya ndege vya Ufaransa.

Yekbun Eksen, mmoja wa wajumbe wa shirikisho la mashirika yanayotetea haki za Wakurdi nchini Ufaransa ameomba jumuiya ya kimataifa kuwapa msaada wa chakula pamoja na kuwawezesha kijeshi raia wa kikurdi wanaojitolea kwa kukapambana na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Wakati huo huo, watu 14 wamefariki jumanne jioni katika makabiliano kati ya waandamanaji wa kikurdi na polisi nchini Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.