Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-IS-Ukimbizi

Kobane: hasira za Wakurdi wa Uturuki dhidi ya Ankara

Baadhi ya raia wa kikurdi wanaunga mkono wapiganaji wa kikurdi, huku wengine wakipandwa na hasira dhidi ya serikali ya Ankara ya kufumbia macho hali inayojiri Kobane.

Makabiliano makali yatokea katika mji wa Diyarbakir kati ya waandamanaji kutoka jamii ya Wakurdi na ploisi.
Makabiliano makali yatokea katika mji wa Diyarbakir kati ya waandamanaji kutoka jamii ya Wakurdi na ploisi. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutolea amri ya kutotembea barabarani katika mikoa mingi ya kusini mashariki mwa Uturuki, hali inaendelea kuwa tata. Polisi katika maeneo hayo wameimarisha ulinzi. Watu watatu wameuawa mapema leo Alhamisi katika.

Hata hivo idadi ya vifo viliyotokea kusini mashariki katika maandamano ya Jumnne wiki hii imetangzwa rasmi kufikia 24.

Jana jumatano, mikusanyiko na makabiliano vimeripotiwa licha ya amri ya kutotembea barabarani kwa muda wa saa 24 iliyotolewa na serikali katika mikoa sita inayokaliwa na Wakurdi karibu na mpaka wa Syria.

Benki maeneo ya kibiashara, Ofisi za posta, ofisi za chama tawala cha AK, baadhi ya majengo ya serikali katika wilaya mbalimbali vimechomwa moto.

Moja ya benki iliyochomwa moto na waandamanaji katika mji wa Diyarbakir nchini Uturuki,Oktoba 8 mwaka 2014.
Moja ya benki iliyochomwa moto na waandamanaji katika mji wa Diyarbakir nchini Uturuki,Oktoba 8 mwaka 2014. REUTERS/Sertac Kayar

Waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, ameitisha Jumatanao wiki hii kikao cha dharura kuhusu jinsi ya kuimarisha usalama, lakini kikao hicho kilidumu saa3, na baadaye Waziri huyo mkuu, alihitimisha kikao hicho akiwataka waandamanaji kusitisha maandamano yao.

Ahmet Davutoglu, ameinyooshea kidole cha lawama jumuiya ya kimataifa kufumbia macho na harakati zinazoendeshwa na utawala wa Bashar Al Assad, akibaini kwamba Syria ndiyo chanzo cha mdororo wa usalama katika Ukanda huo wa Mashariki ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.