Pata taarifa kuu
YEMENI-MAPIGANO-USALAMA

Yemen: mkataba wa kusitisha mapigano waanza katika hali ya wasiwasi

Mkataba wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano uliopendekezwa na rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi umeanza kutekelezwa usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu.

Mpiganaji wa waasi wa Kishia wa Huthi akitoa ulinzi, wakati ambapo raia wa Yemen wakiendelea kuandamana dhidi ya mashambulizi ya Saudi Arabia, Sanaa, Julai 24 mwaka 2015.
Mpiganaji wa waasi wa Kishia wa Huthi akitoa ulinzi, wakati ambapo raia wa Yemen wakiendelea kuandamana dhidi ya mashambulizi ya Saudi Arabia, Sanaa, Julai 24 mwaka 2015. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo imesikika Jumapili Julai 27 kuwa kiongozi wa waasi wa Kishia nchini Yemen, Abdel Malek al - Houthi, ametupilia mbali pendekezo hilo katika ujumbe uliorushwa kwenye mtandao wa intaneti. Taarifa ambayo imekanushwa baadae na msemaji wake.

Taarifa ambayo ilirushwa kwenye akaunti ya Twitter ya kiongozi wa waasi wa Kishia, Abdel Malak al-Houthi imelea shaka na machafuko. Ujumbe uliorushwa hewani Jumapili mchana kwenye akaunti ya Twitter kwa jina la kiongozi wa waasi, ambayo haijathibitishwa lakinini inafuatiliwa na zaidi ya watu 16,000, imeeleza kuwa "pendekezo la kusitisha mapigano limefutiliwa mbali" na kwamba "vita vinaendelea", amearifu mwandishi wetu Riyadh, Clarence Rodriguez.

Msemaji wa kundi la waasi baadae alikanusha taarifa hiyo, huku akithibitisha kwamba kiongozi wake hana akaunti " iwe kwenye Twitter au mitandao mingine ya kijamii". Hata hivyo, mwenyekiti wa "Kamati ya Mapinduzi" amesema kundi lake "halijafahamishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu pendekezo hilo la kusitisha mapigano" ili waweze kutoa msimamo wao. Kwa upande wake rais Hadi ameonya dhidi ya waasi wa kishia wa Huthi dhidi ya "ukiukaji wa pendekezo hilo, watakubali athara zote zitakazotokana na kuvunjika kwa mkataba wa kusitisha mapigano".

Mkataba huo wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano umeleta hali ya wasiwasi na mkanganyiko. Mashirika ya kiutu nchi humo yameendelea kuunga mkono ili mkataba huo uheshimishwe. Mikataba mitau ya kusitisha mapigano iliyotekelezwa katikati ya mwezi wa Mei na Julai 10 haikudumu kwa muda mrefu, na hivyo kupelekea kudhoofika afya ya zaidi mamilioni ya raia wa Yemen ambao wameendelea kuathirika na vita kwa miezi minne sasa.

Kwa mujibu wa mashahidi, Waasi wa Kishia wa Huthi wameshambulia kijiji kimoja kusini mwa Yemen mara baada ya mkataba huo wa kusitisha mapigano kuanza kutekelezwa. Waasi na wanajeshi wamekua wakirushiana risasi kaskazini mwa mji wa Aden, ambako waasi wameendelea kujidhatiti dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya serikali ambavyo vinaushikilia mji huo wa kusini wenye bandari.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameomba waasi kuheshimu mkataba huo wa kusitisha mapigano na kutoa wito kwa pande zinazokinzana "kujizuia na chokochoko na kuepuka ghasia".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.