Pata taarifa kuu
YEMENI-MAPIGANO-USALAMA

Yemen: Aden yaendelea kukabiliwa na vita

Watu arobaini na tatu ikiwa ni raia wa kawaida wameuawa na wengine 112 wamejeruhiwa katika mashambulizi yalioendeshwa Jumapili Julai 19 na waasi wa kishia wa Huthi dhidi ya eneo la Kazskazini la Aden, afisa wa Afya katika mji huo wa kusini mwa Yemen amebaini.

Nchini Yemen, vita ili kudhibiti mji wa Aden vinaendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Huthi.
Nchini Yemen, vita ili kudhibiti mji wa Aden vinaendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Huthi. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo ya roketi aina ya Katyusha na makombora mengine, yanatokea wakati ambapo vikosi vya serikali vinajitahidi kuulinda mji ambao vilithibitisha hivi karibuni kuutwaa kutoka mikononi mwa waasi.

Vita ya Aden vinaonekana kutomalizika hivi karibuni. Jumapili Julai 19, wapiganaji wanaopambana dhidi ya waasi wa Huthi wametangaza kwamba wmeendelea kufanikiwa na sasa wanaelekea yao kuelekea Ikulu. Ikulu inapatikana katika kata moja ya mji wa Aden, ambayo bado inashikiliwa na waasi. Lengo ni kutoa ulinzi katika mji huo wenye bandari.

Siku tatu ziliopita serikali ilio uhamishoni, hata hivyoilitangaza kuwa mji wa Aden "umeondolewa mikononi mwa waasi". Baadhi ya mawaziri walirejea kukagua maeneo yaliyoondolewa mikononi mwa waasi. Mawaziri hao walifanya mkutano Jumamosi mwishoni mwa juma hili kujadili jinsi ya kuulinda mji huo.

Waasi Huthi hawajakubali kushindwa

Lakini waasi wa Kishia wa Huthi hawajakubali kushindwa. waasi hao wammendelea kuusaidiwa na vikosi vya wanajeshi wanaomuunga mkono rais wa zamani Ali Abdullah, huku wakiendelea kujidhatiti vilivyo.

Kaimu mkuu wa mji wa Aden ameshutumu waasi kutekeeza mashambulizi ya mabomu ambayo yamelenga maeneo yanayokaliwa na watu wengi, kaskazini mwa mji wa Aden.

Julai 10, Umoja wa Mataifa ulitangaza kusitishwa kwa mapigano kwa ajili yakuingiza misaada ya kibinadamu katika mji wa aden. Lakini muendelezo wa mapigano kwa miezi minne sasa umesababisha zoezi hilo kutofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.