Pata taarifa kuu
YEMENI-MAPIGANO-USALAMA

Yemen: wanajeshi watiifu kwa serikali waendelea vita dhidi ya waasi

Nchini Yemen, vikosi tiifu kwa serikali vinavyosaidiwa na muungano unaongozwa na Saudi Arabia vimeudhibiti Jumapili Agosti 9 mji wa Zinjibar, mji mkuu wa jimbo la Abyan kusini mwa nchi hiyo. Eneo muhimu linalopatikana kilomita 50 na mji wa Aden. Pigo jingine jipya kwa waasi wa Huthi.

Vikosi vinavyoiunga mkono serikali vikipata usaidizi wa vifaa vya jeshi, ikiwa ni pamoja na vifaru.
Vikosi vinavyoiunga mkono serikali vikipata usaidizi wa vifaa vya jeshi, ikiwa ni pamoja na vifaru. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

imechukua muda wa siku mbili wa kuzingira na kusaidiwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ili vikosi tiifu kwa serikali kuudhibiti mji wa Zinjibar. Wapiganaji wanaomuunga mkono rais Hadi walichukua kwanza udhibiti wa kambi ya Brigade ya 15 ya jeshi la Yemen, ambapo maafisa wa jeshi walikuwa walijiunga na waasi wa Huthi, kabla ya kuingia katika mji na kuwaondoa wapinzani wao.

Ushindi huu ni muhimu. Udhibii wa mji wa Zinjibar utapelekea kambi tiifu kwa serikali ya Yemen kufikia maeneo yanayodhibitiwa na waasi kusini mwa Aden, na kuleta juhudi zake zote katika mji wa Taiz, kaskazini Yemen. Ni ushindi hasa muhimu kwa ari ya vikosi tiifu kwa serikali ya Yemen. Tangu katikati ya mwezi Julai na udhibiti wa mji wa Aden, ni mafanikio ya tatu mfululizo dhidi ya waasi wa Huthi. Siku ya Jumanne wiki hii iliopita, vikosi vinavyoiunga mkono serikali vilichukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa al-Anad, ambao uliku ukidhibitiwa na waasi wa Huthi tangu mwezi Machi mwaka huu.

Waasi wa Huthi wameshindwa kwa sasa kudhibiti mashambulizi ya vikosi tiifu kwa serikali ya Yemen na sasa wanalazimika kupambana wakirudi nyuma katika mikoa ya kaskazini. jambo jingine ambalo limepelekea waasi wanapoteza muelekeo ni kutokana na kupingwa na raia ambao wanawaangalia kwa jicho la hasidi wapiganaji wa Huthi kutoka eneo la kaskazini. "Ari imebadili muelekeo. Nguvu imebadilika kutoka upande mmoja kwenda mwengine. Nguvu hizo kwa sasa ziko upande wa vikosi vinavyoiunga mkono serikali ", Franck Mermier, mkurugenzi wa utafiti katika CNRS na mtaalamu wa nchi ya Yemen, amebaini.

Mashambulizi makubwa yanayoendeshwa kusini mwa Yemen na wanajeshi wanaomuunga mkono rais Hadi yanasaidiwa na mashambulizi ya angani ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia. Mashambulizoi hayo pia yanasaidiwa na uratibu mkuu wa makundi mbalimbali yanayopambana dhidi ya waasi wa Huthis.

" Tuko katika vita vya kudhibiti maeneo yalio chini ya udhibiti wa waasi wa Huthi tukianzia kusini mwa nchi ili kumuwezesha rais Hadi kurudi katika mji wa Aden ", amesema Franck Mermier.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.