Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-SAUDI ARABIA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Stephen O'Brien alaani mashambulizi ya Muungano Yemen

Mkuu wa maswala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien ameshtumu mashambulizi ya angaa yalinaoongozwa na Saudi Arabia katika mji wa Hodeida.

Wapiganaji wanaounga mkono serikali nchini Yemen wakiwa mbele ya kambi ya jeshi ya al-Anad, Agosti 3, 2015.
Wapiganaji wanaounga mkono serikali nchini Yemen wakiwa mbele ya kambi ya jeshi ya al-Anad, Agosti 3, 2015. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa anasema kuwa mashambulizi hayo yamesabisha vyakula, dawa na vitu vingine muhimu vya kibinadamu kutowafikia raia wanaoendelea kuteseka kutokana na machafuko yanayoendelea.

O'Brien, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ameshangazwa na hali ya kibinadamu invyoendelea nchini Yemen.

Vikosi tiifu kwa serikali vinavyosaidiwa na muungano unaongozwa na Saudi Arabia viliudhibiti Jumapili Agosti 9 mji wa Zinjibar, mji mkuu wa jimbo la Abyan kusini mwa nchi hiyo. Eneo muhimu linalopatikana kilomita 50 na mji wa Aden. Pigo jingine jipya kwa waasi wa Huthi.

Mashambulizi makubwa yanayoendeshwa kusini mwa Yemen na wanajeshi wanaomuunga mkono rais Hadi yanasaidiwa na mashambulizi ya angani ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia. Mashambulizi hayo pia yanasaidiwa na uratibu mkuu wa makundi mbalimbali yanayopambana dhidi ya waasi wa Huthis.

Vita hivi vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Yemen vimesababisha vifo vya watu wengi na wengine kulazimika kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.