Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-MAKABILIANO-USALAMA

Makabiliano mapya kati ya polisi wa Israel na Waislam katika Msikiti wa Al Aqsa

Makabiliano mapya kati ya polisi wa Israel na vijana wa Kipalestina yametokea Jumatatu hii asubuhikatika Msikiti mtakatifu wa Al Aqsa mjini Jerusalem, ambapo hali ya taharuki imetanda kufutia maadhimisho ya sikukuu ya Wayahudi ya Sukkot, kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Wanawake wa Kipalestina wakiandamana Septemba 27, 2015 Msikiti wa Al Aqsa, Jerusalem.
Wanawake wa Kipalestina wakiandamana Septemba 27, 2015 Msikiti wa Al Aqsa, Jerusalem. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari polisi wametumwa katika Msikiti baada ya kutumia mabomu ya machozi na mabomu mengine kwa kuwatawanya waumini na vijana waliokua wakiandamana, ambao wamerusha mawe, kabla ya kuweka vizuizi ndani ya Msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa ambao umezingirwa na vikosi vya usalama.

Kwa mujibu wa polisi, waandamanaji, ambao wamelala usiku waJumapili kuamkia Jumatatu katika Msikiti, wamewarushia askari polisi mabomu yaliyotengenezwa kienyeji na mawe, jambo ambalo limesababisha moto kutokea kwenye mlango wa jengo hilo. Katika taarifa, polisi imeshutumu " vitendo vya kijinga katika eneo takatifu ".

" Msikiti wa AlAqsa, eneo la tatu takatifu kwa Waislamu Uislam, ambalo Wayahudi wanalichukulia kama eneo lao takatifu. hali hiyo imekua ikizua makabiliano na machafuko kati ya Watahudi na waislam, kila upande ukitaka kuchukua udhibiti wa eneo hilo.

Waislam wanawatuhumu viongozi wa Israel kwamba wanataka kuchukua udhibiti wa eneo lote la Msikiti huo, tuhuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Israel.

Waislamu waliokuwa katikakatika Msikiti huo baada ya sala ya asubuhi waliondolewa na polisi ambayo ilitangaza Jumapili kuwa ni marufuku kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa hadi itakapotangazwa hatua mpya, ispokua kwa watu wazima walio na zaidi umri wa miaka 50 kwa wanaume, kikomo kilichowekwa mara kwa mara katika kipindi cha mvutano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.