Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Waisrael sita wajeruhiwa, mmoja wa washambuliaji auawa

Waisrael sita wamejeruhiwa Jumapili hii katika mashambulizi matatu yalioendeshwa na Wapalestina, ambapo mmoja wao ameuawa, katika Ukingo wa Magharibi, vyanzo vya Israel vimebaini.

Mpalestina aligonga kwa gari lake dhidi ya kundi la Waisrael karibu kituo cha ukaguzi katika Ukingo wa Magharibi, na kuwajeruhi watatu kati yao.
Mpalestina aligonga kwa gari lake dhidi ya kundi la Waisrael karibu kituo cha ukaguzi katika Ukingo wa Magharibi, na kuwajeruhi watatu kati yao. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yanatokea wakati ambapo Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amejielekeza Mareani Jumapili hii, ambapo atakutana na Rais Barack Obama Jumatatu hii na hasa kujadili mvutano kati ya Israel na Palestina.

Tangu Oktoba 1, machafuko yanayoendelea yamesababisha vifo vya Wapalestina 74, ikiwa ni pamoja na Muisrael mwenye asili ya Kiarabu mmoja na Waisrael tisa katika ardhi ya Palestina na Israel. Idadi kubwa ya Wapalestina wameuawa wakiendesha mashambulizi katika Ukingo wa Magharibi, kwa mujibu wa Israel.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi la Israel, wimbi hili la machafuko mabaya litaendelea kushuhudiwa katika nchi hizi mbili, hasa katika Ukingo wa Magharibi.

" Hali hii itachukua muda mrefu, angalau miezi kadhaa ijayo. Tumejiandaa ipasavyo, na tuko tayari kukabiliana nayo hata kwa muda mrefu ", ametangaza kwenye kituo cha redio inayomilikiwa na jeshi kanal Shomer, mkuu wa kikosi kiliotumwa katika Ukingo wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.