Pata taarifa kuu
YEMENI-SIASA

Yemen: Rais Abd Rabbo Mansur Hadi akabidhi mamlaka yake kwa baraza jipya la urais

Rais wa Yemen ametangaza Alhamisi Aprili 7 kuundwa kwa baraza jipya la rais litakaloongoza nchi hiyo, iliyoathiriwa na vita ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu mwaka 2014 dhidi ya waasi wa Houthi, kimetangaza chombo cha habari cha serikali.

Rais wa Yemen Abd Rabbo Mansur ambaye amekabidhi mamlaka kwa baraza jipya la urais.
Rais wa Yemen Abd Rabbo Mansur ambaye amekabidhi mamlaka kwa baraza jipya la urais. afp.com/Natalia Kolesnikova
Matangazo ya kibiashara

"Ninakabidhi mamlaka yangu kamili kwa baraza hili la rais bila kubatilishwa," Rais Abd Rabbo Mansur Hadi amesema katika taarifa yake kwa njia ya televisheni. Tangazo ambalo linakuja katika siku ya mwisho ya mazungumzo ya amani kuhusu Yemen huko Riyadh.

Baraza hili jipya litaundwa na wajumbe wanane na litaongozwa na Rashad al-Alimi, waziri wa zamani wa mambo ya ndani na mshauri wa Abd Rabbo Mansour Hadi. Serikali ya Abd Rabbo Mansur Hadi - inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa na kuungwa mkono tangu mwaka 2015 na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia - na waasi wa Houthi - wanaoungwa mkono na Iran ambayo wanakanusha kuwapa silaha, wamekuwa wakipigania mamlaka tangu waasi kuchukua mji mkuu Sanaa mwaka 2014.

Makubaliano ya kusitisha vita kwa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani

Mkataba wa usitishwaji mapigano kati ya pande hizimbili ulifikiwa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa na ulianza kutekelezwa Jumamosi - siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa mfungo kwa Waislamu - ukitoa mwanga wa matumaini katika vita ambavyo vimesababisha moja ya machafuko makubwa zaidi ya kibinadamu duniani. Chini ya makubaliano haya mapya, ambayo yanaweza kufanywa upya "kwa ridhaa" ya pande hizo mbili, mashambulizi yote ya kijeshi ya anga, ya ardhini na baharini yanapaswa kusitishwa, katika mzozo huu ambao umesababisha mamia ya maelfu ya watu kupoteza maisha, kulingana na Umoja wa Mataifa, na kusababisha nchi hii maskini katika rasi ya Uarabuni kutishiwa na njaa.

Tangazo la usitishwaji mapigano lilikuja wakati majadiliano juu ya Yemen yalikuwa yakifanyika nchini Saudi Arabia, bila ya waasi, ambao walisema wamekataa kushiriki katika mazungumzo ambayo yanafanyika kwenye ardhi ya "adui".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.