Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Afghanistan: Hamsini na tatu waangamia katika shambulio dhidi ya kituo cha mafunzo

Shambulio la kujitoa mhanga lililofanywa Ijumaa, Septemba 30 lilifanyika katika wilaya ya Kabul wanakoishi Washia walio wachache kutoka jamii ya Hazara wanaochukuliwa kuwa waasi na Taliban. Wasichana waliotenganishwa na wavulana katika chumba hicho ndio waathiriwa wakuu wa shambulio hilo.

Chumba kilichoharibiwa katika eneo la shambulizi la bomu la kujitoa mhanga katika kituo cha mafunzo katika kitongoji cha Dasht-e-Barchi huko Kabul mnamo Septemba 30, 2022.
Chumba kilichoharibiwa katika eneo la shambulizi la bomu la kujitoa mhanga katika kituo cha mafunzo katika kitongoji cha Dasht-e-Barchi huko Kabul mnamo Septemba 30, 2022. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Ijumaa, Septemba 30, shambulio la kujitoa mhanga, ambalo bado halijadaiwa na kundi lolote, lilitekelezwa katika kituo kinachoandaa mitihani ya kuingia chuo kikuu. Shambulio hilo liliua watu 53. Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) ulitaka kuitahadharisha jumuiya ya kimataifa kuhusu ukweli kwamba wengi wa wahanga wa shambulio hili ni wasichana na wanawake. Idadi ya watu 110 waliojeruhiwa inazua hofu kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka zaidi.

Kulingana na mwanafunzi aliyekuwa eneo la tukio wakati wa mlipuko huo, aliyehojiwa na shirika la habari la AFP, "wavulana wachache waliathirika, kwa sababu walikuwa nyuma ya darasa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliingia kupitia mlango wa mbele walipokuwa wameketi wasichana".

Mamlaka ya Taliban, kwa upande wake, inatoa idadi ya watu 25 waliofariki na 33 kujeruhiwa.

Mwishoni mwa juma, maandamano ya hapa na pale yalifanyika katika mji mkuu na miji mingine. Mndamano hayo yalioongozwa na wanawake waliokuja kulaani shambulio hilo na kusema kwamba wataendelea kusoma: “Kitu pekee tulicho nacho ni elimu. Elimu ndiyo silaha yetu, na wanataka kuichukua kutoka kwetu,” mmoja wao aliliambia shirika la habari la AFP. Maandamano haya yalizimwa na wanajeshi wa Taliban ambao walifyatua risasi hewani mara kadhaa kuwatawanya waandamanaji.

Wilaya ya Dasht-e-Barchi ambako shambulio hilo lilitokea imeathirika pakubwa katika miaka ya hivi karibuni, na tangu kurejea madarakani kwa Taliban, na mashambulizi yaliyodaiwa na tawi la kikanda la kundi la wanajihadi la Islamic State, EI- K, ambalo linawachukulia watu kutoka jamii ya Hazaras kama wazushi.

Tangu Taliban waingie madarakani mwezi wa Agosti 2021, wameweka kanuni kali kuhusu elimu ya wasichana ambao hawawezi tena kupata elimu ya sekondari. Kwa upande mwingine, wanafunzi wa kike wanapokelewa chuo kikuu, lakini idadi yao inapaswa kupungua kadri miaka inavyokwenda, kwa kukosa kwenda shule ya upili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.