Pata taarifa kuu

Afghanistan: Marufuku wanawake kusoma chuo kikuu Afghanistan

Mamlaka ya Taliban imetangaza tangu Jumanne kwamba vyuo vikuu vya Afghanistan sasa vimepigwa marufuku kwa wanawake kwa muda usiojulikana, ambao tayari wamenyimwa elimu ya sekondari nchini Afghanistan, tangu kuingia madarakani kwa kwa Waislamu wenye itikadi kali za kidini.

Wanafunzi wakiwa mbele ya Chuo Kikuu cha Kabul nchini Afghanistan, tarehe 26 Februari 2022.
Wanafunzi wakiwa mbele ya Chuo Kikuu cha Kabul nchini Afghanistan, tarehe 26 Februari 2022. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya wanafunzi walijaribu kufika chuo kikuu siku ya Jumatano asubuhi, lakini kadhaa kati yao walilakiwa na vipigo kutoka kwa wanajeshi wa Taliban wanaosimamia usalama kwenye milango ya vyuo vikuu, anaripoti mwandishi wetu katika mkoa huo, Sonia Ghezali.

Mamlaka ya Taliban mnamo Jumanne (tarehe 20 Desemba) iliamuru kupiga marufuku elimu ya chuo kikuu kwa wanawake "kwa muda usiojulikana". "Nyote mnaarifiwa kutekeleza agizo lililotolewa la kusimamisha elimu ya wanawake hadi itakapochukuliwa hatua nyingine," Waziri wa Elimu ya Juu, Neda Mohammad Nadeem alisema katika barua iliyotumwa kwa vyuo vikuu vyote vya serikali na vya kibinafsi nchini, siku ya Jumanne, Desemba 20.

'Ninaogopa sana wakati ujao wenye giza unaotungojea'

“Niliposikia habari hizo sikuweza kujizuia kulia,” anasema Laila, mwanachuoni katika menejimenti na usimamizi wa biashara. Hakuna mwalimu wake yeyote katika chuo kikuu anachosoma huko Herat aliyemwonya. Alipata habari hiyo kwenye vyombo vya habari, alishangaa na kufadhaika.

"Nina hofu na mustakabali wenye giza unaotungoja," anapumua Rabia, mwanafunzi katika masuala ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Kabul. "Siwezi kuamua maisha yangu ya baadaye, wengine wanafanya kwa niaba yangu," anajuta bila msaada. Hata hivyo, amesema hawezi kukata tamaa. Anahakikisha kwamba ataendelea kujifunza nyumbani.

Bado hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kuhalalisha uamuzi huu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema "amefadhaika sana" na kuwataka Taliban "kuhakikisha upatikanaji sawa wa elimu katika ngazi zote", kulingana na msemaji wake. Marekani inashutumu "uamuzi wa kikatili".

Shahrzad Akbar, mkuu wa zamani wa Tume Huru ya Haki za Kibinadamu nchini Afghanistan, akiwa uhamishoni nje ya nchi, amejibu kwenye Twitter: "Chini ya utawala wa Taliban, Afghanistan imekuwa kaburi la matumaini na ndoto za Waafghanistan.

Marufuku ya elimu ya juu inajiri chini ya miezi mitatu baada ya maelfu ya wasichana na wanawake kufanya mitihani ya kujiunga na chuo kikuu kote nchini. Wengi wao walitamani kuchagua kati ya taaluma ya uhandisi au udaktari, ingawa walinyimwa fursa ya kwenda shule za upili.

(Pamoja na AFP)na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.