Pata taarifa kuu

Matetemeko ghanistan: Zaidi ya elfu mbili wafariki, shughuli za uokoaji zinaendelea

Kulingana na ripoti rasmi ya hivi punde, zaidi ya watu 2,000 wamefariki katika tetemeko kubwa la ardhi lililopiga magharibi mwa Afghanistan Jumamosi hii, Oktoba 7, na kusababisha uharibifu mkubwa. Zaidi ya watu 9,200 wamejeruhiwa na karibu nyumba 1,300 kuharibiwa au kusombwa. Shughuli za uokoaji zinaendelea kutafuta manusura katika magofu ya vijiji vilivyoathirika.

Wakazi wakiondoa mabaki ya nyumba zao zilizoharibiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi katika wilaya ya Zendeh Jan, magharibi mwa Afghanistan, Oktoba 7, 2023.
Wakazi wakiondoa mabaki ya nyumba zao zilizoharibiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi katika wilaya ya Zendeh Jan, magharibi mwa Afghanistan, Oktoba 7, 2023. AFP - MOHSEN KARIMI
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha Richter, likifuatiwa na mitetemeko minane yenye nguvu baada ya tetemeko hilo, ni mojawapo ya matukio mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka ishirini. Jumapili hii, mmoja wa wasemaji wa serikali amesema kuwa zaidi ya watu 2,050 wamefariki katika vijiji 13, watu 9,240 wamejeruhiwa na kwamba timu kumi za uokoaji zimefika eneo la tukio.

Shughuli za uokoaji zinaendelea. Watu bado wamenasa kwenye vifusi katika vijiji vilivyoathiriwa zaidi, anaripoti mwandishi wetu wa kikanda, Sonia Ghezali. Kutakuwa na makumi ya vijiji vilivyoharibiwa kabisa au kiasi. Mamlaka ya Taliban imetangaza leo Jumapili asubuhi kwamba waathiriwa walikuwa na uhitaji wa haraka wa chakula, maji, dawa na mahema. Zaidi ya miili 200 imepelekwa hospitali katika mkoa huo, afisa wa mamlaka ya afya huko Herat amesema.

Katika vijiji vya wilaya iliyoathiriwa zaidi, Zendeh Jan, ambayo ni kitovu cha tetemeko la ardhi, kilomita 40 kutoka mji wa Herat, mamia ya nyumba zimeanguka, nyumba ambazo zilijengwa kwa udongo. Kwa mujibu wa mfanyakazi wa zamani wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini Afhganistan, hivi ni vijiji maskini zaidi, ambapo wakaazi wanapata riziki kutokana na kupanda zabibu. Vijiji ambavyo vimeathiriwa sana na ukame ambao umeikumba sehemu hii ya Afghanistan kwa miaka kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.