Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Shambulio la Oktoba 7: Familia tisa za raia wa Israel zawasilisha malalamiko kwa ICC

Wakili François Zimeray, raia wa Ufaransa, ametangaza siku ya Ijumaa kwamba amewasilisha malalamiko yake kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Imeamriwa na familia tisa za wahanga wa Israeli wa shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7.

Majengo ya ICC.
Majengo ya ICC. Peter Dejong/AP/SIPA - Peter Dejong/AP/SIPA
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na François Zimeray, shambulio lililotekelezwa Oktoba 7 na Hamas nchini Israel "ni utekelezaji wa mradi wa mauaji ya halaiki uliotangazwa na wahusika wa shambulio hilo". Na "kutokana na kukataa kwa wakati halisi, ukweli lazima ulindwe, ukatili huu lazima ujulikane na kuandikwa katika kumbukumbu ya pamoja," amebainisha. Pia anamwomba mwendesha mashtaka wa ICC "kuzingatia ushauri wa kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa viongozi wa Hamas," kulingana na taarifa.

Wakili huyo aligeukia ICC, kwa sababu ndiyo "mrithi" wa kesi ya Nuremberg. "Hili ndilo jambo bora zaidi ambalo jumuiya ya kimataifa imejenga ili kukabiliana kwa usahihi na ukatili mkubwa." Mahakama ilithibitisha kupokea faili kutoka kwa wakili wa Ufaransa.

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa ICC imesema itapitia taarifa hizo ili kuona kama uhalifu unaodaiwa kuwa unawezekana uko chini ya mamlaka ya mahakama hiyo na unaweza kuhusishwa na uchunguzi wake unaoendelea kuhusu hali ya Palestina. Hata hivyo, mahakama hiyo iliyoko Hague, hailazimiki kuishughulikia.

François Zimeray amepewa mamlaka na familia tisa za wahanga wa Israeli. Raia wote, "kadhaa walikuwa kwenye karamu ya rave party "Tribe of Nova", tamasha la muziki, mahali pa mikutano na amani katika jangwa la Negev," ameongeza. Tarehe 7 Oktoba, zaidi ya watu 250 waliuawa na wanachama wa tawi la kijesi la kundi la wanamgambo la Palestina wakati wa shambulio kwenye tamasha hili la muziki ambalo lilifanyika kilomita chache kutoka Ukanda wa Gaza.

Kwa jumla, zaidi ya watu 1,400, hasa raia, waliuawa katika shambulio la Oktoba 7, kulingana na mamlaka ya Israeli. Na tangu shambulio hilo, Israel imeshambulia bila kuchoka Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa Ijumaa na Hamas, watu 9,227, wakiwemo watoto 3,826, wameuawa katika mashambulizi ya Israel katika eneo hilo.

Majibu ya Israel pia yanachunguzwa kwa karibu na ICC. Mkuu wa ICC, Karim Khan, alisema "anachunguza uhalifu ambao unaweza kuwa ulifanywa nchini Israel mnamo Oktoba 7" lakini pia "matukio yanayoendelea huko Gaza na Ukingo wa Magharibi" kama sehemu ya uchunguzi rasmi wa ICC uliofunguliwa mnamo 2021 kwenye maeneo ya Palestina. Zaidi ya hayo, Mahakama hiyo pia iliombwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Reporters Without Borders kwa uhalifu wa kivita uliofanywa dhidi ya waandishi wa habari nchini Palestina na Israel.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.