Nchi tano zawasilisha malalamiko yao ICC kufuatia mashambulizi ya Israel katika eneo laPalestina
Nchi tano miongoni mwa nchi zilizotia saini kuhusu kuundwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) zimeomba kufanyika kwa uchunguzi kuhusu hali katika eneo la Palestina kufuatia mashambulizi ya Israel yanayoendelea.
Imechapishwa:
Hayo yametaganzwa na Mwendesha wa mahakaam hiyo, ambaye amebainisha kuchunguza kuhusu uhalifu uliofanywa tangu shamblio baya la hamas la Octoba 7 baada ya kupata malalamiko kutoka Afrika Kusini, Bangladesh, Bolivia, Comoro na Djibouti.
Afrika Kusini imeeleza kuwa imewasilisha malamiko haya na "nchi nyingine zinazotiwa wasiwasi na hali hii huko Palestina", ili ICC ichukuwe "hatua ya haraka kwa uzito wa hali ya sasa".
UNRWA yatangaza shambulio jipya la bomu kwenye mojawapo ya shule zake
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini amebainisha kwenye mtandao wa X (zamani ikiitwa Twitter) kwamba shule ya pili imelengwa, hii ni mara ya pili chini ya saa ishirini na nne. Shambulio la kwanza lilitokea katika kambi ya Jabaliya Jumamosi asubuhi.