Pata taarifa kuu

Mkuu wa Umoja wa Afrika 'akaribisha' uamuzi wa ICJ kuhusu Mashariki ya Kati

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, siku ya Jumamosi amekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, ambayo iliitaka Israel kuzuia kitendo chochote kinachowezekana cha "mauaji ya kimbari" huko Gaza.

Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Uamuzi huo unathibitisha kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa na hitaji la Israeli kufuata ipasavyo majukumu yake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari," Bw. Faki amesema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii. Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini Hague ilitoa uamuzi wake wa kwanza siku ya Ijumaa katika kesi hii ya kihistoria kwa mpango wa Afrika Kusini, mwanachama wa Umoja wa Afrika.

Israel lazima "ichukue hatua zote katika uwezo wake" kuzuia kitendo chochote cha mauaji ya kimbari na hakuna kiongozi anayepaswa kutoa matamshi ya kuchochea mauaji ya halaiki, mahakama ilisema. Mbali na hayo, "Taifa la Israel lazima lichukue hatua madhubuti mara moja ili kuwezesha utoaji wa huduma za kimsingi na misaada ya kibinadamu," iliongeza.

Afrika Kusini iliishutumu Israel kwa kukiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1948 (ulioanzishwa kufuatia Vita vya Pili vya Dunia na Holocaust) wakati wa kampeni yake ya kijeshi huko Gaza, iliyoanzishwa na Hamas katika ardhi ya Israeli mnamo Oktoba 7.

Mahakama haikutoa uamuzi iwapo Israel ilikuwa ikifanya mauaji ya halaiki. Ilitoa maagizo ya dharura kabla ya kukagua kesi hiyo kwa uhalali wake, mchakato unaotarajiwa kuchukua miaka kadhaa. Bw. Faki amesema Umoja wa Afrika umekaribisha hatua zilizoamriwa na Mahakama.

Vita huko Gaza vilianza na shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7, ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,140 nchini Israeli, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP likijikita kwa takwimu rasmi za Israeli. Wanamgambo hao pia walichukua karibu mateka 250 na Israel inasema karibu 132 kati yao wamesalia Gaza, ikiwa ni pamoja na miili ya mateka 28 walioaga dunia.

Israel iliapa kuiangamiza Hamas na kuanzisha mashambulizi ya kijeshi ambayo, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza, yalmesababisha vifo vya watu 26,257, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na vijana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.