Pata taarifa kuu

Iran inaitaka FIFA kuifungia Israel kushiriki shughuli zake

Nairobi – Shirikisho la kandanda la Iran limetoa wito kwa shirikisho la soka duniani FIFA, kuzuia shirikisho la soka la Israel kushiriki katika shughuli zote zinazohusiana na soka kutokana na vita vya nchi hiyo huko Gaza.

Nembo ya shirikisho la soka duniani FIFA
Nembo ya shirikisho la soka duniani FIFA AP - Alessandro Della Bella
Matangazo ya kibiashara

Mapigano katika Ukanda wa Gaza yalianza tarehe 7 Oktoba mwaka uliopita baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio dhidi ya Israel.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya takriban watu 1,160, wengi wao wakiwa raia kwa mujibu wa takwimu rasmi za Israeli.

Kutokana na shambulio hilo, Israel iliapa kulimaliza kundi la Hamas ambapo ilianzisha mashambulio ya angani na ardhini ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu 27,947, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, kulingana na wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza inayoendeshwa na Hamas.

Israel imeapa kulimaliza kundi la wapiganaji wa Hamas
Israel imeapa kulimaliza kundi la wapiganaji wa Hamas AFP - MAHMUD HAMS

Iran imedai kuwa  shambulio  la Hamas la Oktoba 7 lilikuwa lenye mafanikio lakini imekana kuhusika moja kwa moja.

Mamlaka ya Iran mwezi Agosti mwaka jana ilimzuia kushiriki michezo Mostafa Rajaei, mchezaji wa kunyanyua vitu vizito, baada ya kusalimiana na mshindani wa Israel katika hafla moja nchini Poland, vyombo vya habari vya serikali viliripoti wakati huo.

Shirikisho la kunyanyua vitu vizito la Iran pia limemfuta kazi mkuu wa ujumbe wa mashindano hayo, Hamid Salehinia.

iongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
iongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei AP

Mnamo 2021, kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliwahimiza wanariadha wa nchi yake kutowasalimu wale aliowataja kama wawkilishi wa utawala wa kihalifu wa (Israeli) ili kupata medali.

Kundi la vyama vya soka vya mashariki ya kati, ikiwa ni pamoja na Palestina, Saudi Arabia, Qatar, na Umoja wa Falme za Kiarabu, pia vimewataka wakuu wa soka duniani kuipiga marufuku Israel kushiriki shughuli zake kutokana na vita vyake dhidi ya Hamas huko Gaza, Sky News iliripoti Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.