Pata taarifa kuu

Vita Gaza: Bunge la Ulaya lataka kusitishwa kwa mapigano mara moja kwa mara ya kwanza

Bunge la Ulaya limepiga kura leo Alhamisi Machi 14 kuunga mkono azimio kuhusu hali ya Gaza na ukweli kwamba kuna hatari njaa kuyakumba maeneo yote ya ukanda wa Gaza. Bunge, kwa kuzingatia kwamba Israel imeimarisha hatua yake ya kuzingira Gaza na inazuia uendeshaji mzuri wa shughuli za kibinadamu, huku ikiendelea na ukoloni, kwa hiyo linatoa wito kwa mara ya kwanza kusitishwa kwa mapigano mara moja.

Wapalestina wakiwa mbele ya jengo la makazi lililoharibiwa na mashambulizi ya Israel huko Rafah, katika Ukanda wa Gaza, Machi 9, 2024.
Wapalestina wakiwa mbele ya jengo la makazi lililoharibiwa na mashambulizi ya Israel huko Rafah, katika Ukanda wa Gaza, Machi 9, 2024. AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Strasbourg, Romain Lemaresquier

Kwa hakika sio azimio hili litakalobadilisha hali ya mambokwa sasa, lakini ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo Bunge la Ulaya kupiga kura juu ya aina hii ya azimio. Azimio hili limewagawanga wabunge wa Umoja wa Ulaya na ni vigumu kupata maelewano. Azimio lililopitishwa leo linalaani kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu na mashambulizi dhidi ya misafara ya kibinadamu na kutoa wito kwa Israel kuidhinisha mara moja na kuwezesha uwasilishaji wa misaada kupitia maeneo yote yenye barabara zinzoingia Gaza.

Bunge la Ulaya pia linalaani mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia na dhidi ya miundo ya kibinadamu na kusikitishwa na matokeo ya janga la hivi karibuni, hasa kwa watoto. Wabunge wanataka kufunguliwa kwa uchunguzi huru wa kimataifa na kuanzisha upya wito wao wa kusitisha mapigano mara moja na ya kudumu. Baraza la Ulaya linatangaza kuwa lina wasiwasi mkubwa na hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza, haswa na hatari ya njaa inayokaribia.

Wabunge hao wameitaka Israel kuheshimu masharti ya sheria za kimataifa za kibinadamu na kuzingatia maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hatimaye, Bunge linasisitiza kwamba kila kitu ni lazima kifanyike ili kuepusha wahanga zaidi wa raia wasio na hatia na kumwagiza Rais wake, Roberta Metsola, kuwasilisha andiko hili kwa Baraza, Tume, Umoja wa Mataifa, Serikali ya Israel na Mamlaka ya Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.