Pata taarifa kuu
SOKA-LIGI YA MABINGWA

Ligi ya Mabingwa: PSG yaipiku Manchester City

Klabu ya Paris Saint-Germain imejilipiza kisasi kwa kushinda mabao 2-0 huko Parc des Princes dhidi ya klabu ya Uingereza ya Manchester City. 

Bao la kwanza la PSG lilifungwa na mchezaji Idrissa Gueye katika dakika ya 8 ya kipindi cha kwanza. Bao la pili liliwekwa wavuni na Lionel katika dakika ya 74 ya mchezo huo (kipindi cha pili).
Bao la kwanza la PSG lilifungwa na mchezaji Idrissa Gueye katika dakika ya 8 ya kipindi cha kwanza. Bao la pili liliwekwa wavuni na Lionel katika dakika ya 74 ya mchezo huo (kipindi cha pili). FRANCK FIFE AFP
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Ufaransa ya Paris Saint Germain (PSG) imefanya kazi kubwa katika mechi ya Jumanne wiki hii. Miezi michache baada ya kufungwa mabao 2-0 na Manchester City na kuondolewa katika nusu fainali ya C1, Paris Saint-Germain imejilipiza kisasi kwa klabu hii ya Uingereza ya Pep Guardiola huko Parc des Princes.

Wakiongozwa na wafungaji wa mabao Idrissa Gueye na Lionel Messi, PSG walipata ushindi dhidi yaMachester City ambao hawakuweza hata kuweka wavuni bao la kufuta majonzi.

Klabu ya Paris Saint Germain pia walichukua fursa ya kuongoza katika msimamo wa kundi A, mbele ya klabu ya Bruges, mshindi (1-2) wa RB Leipzig.

Bao la kwanza la PSG lilifungwa na mchezaji Idrissa Gueye katika dakika ya 8 ya kipindi cha kwanza. Bao la pili liliwekwa wavuni na Lionel katika dakika ya 74 ya mchezo huo (kipindi cha pili).

Hata hivyo baada ya bao la kwanza la PSG, Manchester ilijaribu kusawazisha bila mafaanikio. Ilitawala mpira kwa 54 %.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.