Pata taarifa kuu
AFCON 2023

Kocha wa Morocco, Regragui apunguziwa adhabu na CAF

Abidjan, Cote D'Ivoire – Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui amepunguzwa adhabu yake na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) na sasa atakuwa kwenye benchi dhidi ya Afrika Kusini katika hatua ya 16 bora.

Kocha wa Morocco Walid Regragui na mchezaji Hakim Ziyech baada ya ushindi dhidi ya Tanzania
Kocha wa Morocco Walid Regragui na mchezaji Hakim Ziyech baada ya ushindi dhidi ya Tanzania © FRMF
Matangazo ya kibiashara

Bodi ya nidhamu ya CAF, mnamo Jumatano 24 Januari 2024, ilitoa uamuzi kuhusu suala linalohusisha shirikisho la soka nchini Morocco (FRMF) na la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FECOFA) kufuatia matukio ya baada ya mechi wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Moroco na Kongo, Jumapili tarehe 21 Januari 2024.

Kocha Walid alipatikana na hatia kwa mashtaka tofauti na kutozwa faini ya dola 5,000 na kufungiwa mechi nne, mbili kati ya hizo zikisimamishwa kwa muda wa mwaka mmoja.

CAF pia iliitoza FRMF na FECOFA faini ya dola 20,000 kila mmoja lakini shirikisho la Moroco likatozwa faini nyingine ya dola 10,000 kwa kutumia mabomu ya moshi na wafuasi wake wakati wa mechi. Dola 5,000 ya kiasi hiki imesimamishwa.

Wachezaji wa akiba wa Morocco wakiimba wimbo wa taifa kabl y kupambana na Zambia uwanjani Laurent Pokou, San Pedro
Wachezaji wa akiba wa Morocco wakiimba wimbo wa taifa kabl y kupambana na Zambia uwanjani Laurent Pokou, San Pedro © EnMaroc

CAF awali ilitangaza kuwa maamuzi hayo yangeanza kutekelezwa baada ya muda wa kukata rufaa kuisha kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za CAF.

Katika taarifa waliyoitoa, FRMF ilielezea uamuzi wa CAF kama "usioeleweka" kwa sababu "ukweli ni kwamba kocha Regragui hakukiuka maadili ya kucheza kwa haki".

Regragui alikosa mchezo wa mwisho wa Kundi F ambao Morocco walishinda 1-0 dhidi ya Zambia siku ya Jumatano. Kocha msaidizi Rachid Benmahmoud alichukua nafasi ya Regragui kwenye benchi la ufundi katika mechi hiyo.

Ila sasa Regragui, atahudhuria mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Afrika Kusini siku ya Jumanne wiki ijayo baada ya rufaa ya shirikisho la soka la Morocco kufanikiwa.

Simba hao wa jangwani waliingia kwenye Afcon ya mwaka huu kama moja ya timu zinazopendekezwa kushinda taji baada ya kuwa timu ya kwanza ya Kiafrika kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia huko Qatar mwaka 2022.

Morocco ilimaliza nafasi ya kwanza kwenye Kundi F kwa alama saba baada ya kushinda Tanzania 3-0, kutoka sare na DRC 1-1 kisha kuifunga Zambia 1-0. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.