Pata taarifa kuu
UFARANSA-UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA

Ufaransa: raia 3 wa Marekani na 1 wa Uingereza watunukiwa zawadi nono

Wanajeshi watatu wa Marekani na mmoja wa Uingereza wametuzwa nishani ya heshima na rais wa Ufaransa François Hollande kwa kufanikiwa kumkamata na kumzuia gaidi aliyekuwa anapanga kutekeleza shambulizi la bomu ndani ya treni ya abiria.

Kutoka kushoto kwenda kulia karibu ya Rais Hollande: raia kutoka Uingereza Chris Norman, raia wa Marekani Anthony Sadler, Spencer Stone na Alek Skarlatos, Agosti 24, 2015 katika Ikulu ya Elysée.
Kutoka kushoto kwenda kulia karibu ya Rais Hollande: raia kutoka Uingereza Chris Norman, raia wa Marekani Anthony Sadler, Spencer Stone na Alek Skarlatos, Agosti 24, 2015 katika Ikulu ya Elysée. REUTERS/Michel Euler/Pool
Matangazo ya kibiashara

Raia hao Spencer Stone, Alek Skarlatos, Anthony Sadler na Chris Norman walimzidi nguvu mlipuaji huyo wakati alipokuwa akijiandaa kutekeleza shambulizi hilo siku ya Ijumaa wiki iliyopita jijini Paris.

Ayoub al-Khazzani bado anaendelea kusikilizwa katika makao makuu ya SDAT, kitengo cha polisi kinachopambana na Ugaidi katika mji wa Levallois-Perret.

Baada ya siku mbili akiwa chini ya ulinzi, Jumapili Agosti 23 Ayoub al-Kazzani alikanusha nia yoyote ya kigaidi. Mtuhumiwa huyo raia wa Morocco, mwenye umri wa miaka 25 anaweza kuendelea kuwa chini ya ulinzi hadi Jumanne wiki hii.

Rais Hollande amewasifia wanajeshi hao kwa kuonesha ujasiri wa hali ya juu.

Ufaransa ni miongoni mwa mataifa ya Ulaya yanayoendelea kupata vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa makundi kama Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.