Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-IS-KOBANE-Ushirikiano-Mapigano-Usalama

Marekani yaishinikiza Uturuki kuanzisha vita dhidi ya IS

Mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kislamu yanaendelea, wakati wapiganaji hao wakiendelea kudhibiti baadhi ya maeneo.

Jenerali John Allen (wapili kutoka kulia) mjumbe maalum wa Marekani nchini Uturuki.
Jenerali John Allen (wapili kutoka kulia) mjumbe maalum wa Marekani nchini Uturuki. REUTERS/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa kimataifa dhidi ya wapiganaji hao wa Dola la Kiislam wameanza kushauriana na Uturuki kwa kuanzisha mashambulizi ya ardhini, baada ya Uturuki kubaini kwamba haiwezi kuanzisha mashambulizi ardhini peke yake.

Mkuu wa muungano wa kimataifa dhidi ya ugaidi, jenerali John Allen, yuko ziarani nchini Uturuki ili kuishawishi serikali ya Uturuki kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam katika mji wa Kobane, ambao uko mbioni kudhibitiwa na wapiganaji hao.

Kwa upande wake Washington, imesema kuna umuhimu wa kuzidisha mashambulizi, kwani wapiganaji wa Dola la Kiislam wanakaribia kuudhibiti mji wa Kobane, licha ya mashambulizi yaliyotekelezwa tangu usiku wa Alhamisi hadi Ijumaa wiki hii. Wapiganaji wa kikurdi wanaendelea kupoteza baadhi ya maeneo kutokana na kuzidiwa nguvu na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Hayo yakijri pendekezo la nchi ya Uturuki kutaka kuwekwa kwa makataa ya anga nchini Syria ili kunusuru mauaji ya raia wasio na hatia, hatimaye limeanza kupata uungwaji mkono toka kwa Serikali ya Marekani.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry, amesema kuwa suala la kuwekwa kwa makataa ya anga nchini Syria ni pendekezo la msingi ambalo kabla ya utekelezwaji wake kunapaswa kuwa na tathmini ya kina kuhusu madhara yanayoweza kutokea iwapo makataa hiyo itatekelezwa.

Waziri Kerry hakupinga moja kwa moja pendekezo hili la Uturuki lakini akataka kuwepo kwa muda zaidi wa kulitazama kabla ya kutekelezwa wakati huu akisema wananchi wa Syria bado wanahitaji msaada mkubwa toka jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.