Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-MAKABILIANO-USALAMA

Mji wa kale wa Jerusalem wazingirwa na vikosi vya Israel

Jeshi la Israel siku ya Jumapili mwishoni mwa Juma hili lililopita limemuua kijana mmoja, raia wa Palestina katika mji wa wa kale wa Jerusalem unaokaliwa na Wayahudi ambako kulitokea makabiliano kati ya vijana wa Palestina na askari wa Israel katika maeneo kadhaa, wakati Waziri Mkuu wa Israel alisema kuanzisha vita ya moja kwa moja dhidi ya " ugaidi wa Kipalestina".

Tangu Alhamisi usiku, maandamano ya kila siku katika Ukingo wa Magharibi, mji wa kale wa Jerusalem. Jumapili Oktoba 4, kumetokea makabiliano kati ya Wapalestina na jeshi la Israel karibu na mji wa Ramallah.
Tangu Alhamisi usiku, maandamano ya kila siku katika Ukingo wa Magharibi, mji wa kale wa Jerusalem. Jumapili Oktoba 4, kumetokea makabiliano kati ya Wapalestina na jeshi la Israel karibu na mji wa Ramallah. REUTERS/Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

Houzeifa Othman Suleiman, mwenye umri wa miaka18, ni raia wa Palestina wa kwanza kuuawa katika makabiliano tangu kuanza machafuko mapya yaliyoenea katika eneo nzima la mji wa kale wa Jerusalem baada ya raia wanne wa Israel kuuawa tangu Alhamisi usiku wiki iliyopita.

Kifo cha Houzeifa Othman Suleiman kinatishia kuibuka kwa vurugu ambazo tayari zimesababisha, kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu, zaidi ya watu 150 kujeruhiwa kwa risasi za chuma au za risasi mpira zinazorushwa na jeshi la Israel.

Katika wiki hiyo, raia wanne wa Israel waliuawa: Walowezi wawili wa Kiyahudi waliuawa kwa risasi Alhamisi usiku mbele ya watoto wao kaskazini mwa mji wa wa kale wa Jerusalem, na watu wawili Jumamosi usiku katika Mji huo mkongwe wa Jerusalem.

Wakati huo huo polisi wa Israeli wametangaza marufuku ya kuingia kwenye mji wa kale wa Jerusalem hatua ambayo itasababisa wapalestina kutoruhusiwa eneo hilo kwa siku mbili.

Wapalestina hawaruhusiwi kuingia eneo hilo isipokuwa wale wanaoishi huko.
Hata hivyo Waisraeli na wamiliki wa biashara pamoja na wanafunzi pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.