Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-Mapigano-Usalama

Somalia: wapiganaji wa Al Shabab wajidhatiti upya

Wanamgambo wa Al Shabab wameanza kujidhatiti upya baada ya kukiteka kisiwa muhimu cha Kudhaa, kusini magharibi mwa Somalia.

Kisiwa cha Kudhaa (kwenye picha hii), ambacho kinadhibitiwa kwa sasa na kundi la Al Shabab.
Kisiwa cha Kudhaa (kwenye picha hii), ambacho kinadhibitiwa kwa sasa na kundi la Al Shabab. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo hao walienseha mashambulizi Jumamosi Novemba 8, na kufanikiwa kudhibiti upya ngome waliyopoteza wiki moja iliyopita.

Kisiwa cha Kudhaa, kiko kilomita 45 kusini magharibi ya Kismayo,na ni moja ya maeno yanayo kuza uchumi wa kundi la Al Shabab.

Wanamgambo wa kiislam wa Al Shabab wamekua wakinufaika kupitia kisiwa hicho kwa kuendesha moja ya shughuli zao kuu za kiuchumi , hususan kuuza makaa. Hivi karibuni utawala wa jimbo la Jubaland na majeshi ya Amisom walitangaza kwamba walirejesha kisiwa hicho mikononi mwa utawala.

Kiongozi mmoja mashuhuri katika kisiwa cha Kudhaa amelimbia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba wapiganaji wa Kiislam walishambulia Jumamosi Novemba 8 kisiwa hicho na kuwatimua wanajeshi wa serikali.

Mkazi mmoja wa Kudhaa amethibitisha kuondoka kwa wanajeshi Jubaland katika kiiswa hicho, huku akibaini kwamba aliona kwa jicho lake "maiti katika mitaa" ya kijiji cha Kudhaa. Hili ni shambulio kubwa la kijeshi kutokea tangu alipouawa kiongozi wa kundi la Al Shabab Ahmed Abdi Godane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.