Pata taarifa kuu
UN-SUDANI-DARFUR-HAKI ZA BINADAMU-SHERIA

Sudani: jeshi lataka kuficha ukweli kuhusu ubakaji

Jeshi la Sudani linadaiwa kuwafanyia vitisho mashahidi wa vitendo vya ubakaji viliyotekelezwa na wanajeshi kwa wanawake 200 katika kijiji cha Darfur ya Kusini mwezi Oktoba uliyopita.  

wanajeshi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Sudani, wakijaribu kuendesha uchunguzi kuhusu vitendo vya ubakaji, lakini mashahidi wakabiliwa na vitisho.
wanajeshi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Sudani, wakijaribu kuendesha uchunguzi kuhusu vitendo vya ubakaji, lakini mashahidi wakabiliwa na vitisho. AFP/ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti ya ndani ya umoja wa Mataifa, vikosi vya Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika havikuweza kufanya uchunguzi katika mazingira mazuri kuhusu tuhuma za ubakaji dhidi ya wanajeshi wa Sudani.

Tume ya Umoha wa Mataifa nchini Sudani imethibisha kwa mashahidi wamekua wakifanyia vitisho, na kulazimika kukaa kimya.

Inaarifiwa kuwa wanawake na wasichana 200 walibakwa na wanajeshi wa sudani. Tume ya mseto ya Umoj awa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbp la Darfour imefanya uchunguzi hivi karibuni katika kijiji cha Tabit, kufuatia taarifa mtandao mmoja wa Sugani ulikua ukithibitisha hali hiyo.

Awali viongozi wa Kijeshi wa Sudani waliwakataza wachunguzi kufika kwenye eneo la tukio. Lakini muda mchache baadae, mlango ulufungulia. Hata hivyo inadhaniwa kuwa watu ho walifyanyia vitisho ili wasithubutu kusema kile waichokona.

Kwa muda wote waliyokua wakiendesha uchunguzi katika kijiji cha Tabit, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika waliwaona wanajeshi wengi Sudan, baadhi walikua wakirekodi mahojiano ya raia wa kijiji hicho na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.