Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-BASHAR-ICC-SHERIA

Afrika Kusini: Serikali yakanusha mpango wa kumtorosha Bashir

Serikali ya Afrika Kusini imevunja ukimya wake baada ya sakata la Omar al-Bashir. Wiki iliyopita, rais wa Sudan aliondoka kimya kimya Afrika Kusini kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Umoja wa Afrika, nchini Afrika Kusini.

Rais wa sudan, Omar Al Bashir, akiwasili Khartoum, Juni 15 mwaka 2015, akitokea Johannesburg.
Rais wa sudan, Omar Al Bashir, akiwasili Khartoum, Juni 15 mwaka 2015, akitokea Johannesburg. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Shirika lisilo la kiserikali la haki za binadamu liliomba haraka vyombo vya sheria vya Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan anayetafutwa na Mahakama ya kimataifa ya ICC kwa tuhuma za mauaji ya kimbari katika vita viliyotokea Darfur.

Omar al-Bashir anakabiliwa na hati mbili za kukamatwa kutokana za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma za mauaji ya kimbari. Serikali imeikanusha Jumatatu hii Juni 22 kwamba ilimtorosha rais wa Sudan, na hivyo kuweza kukwepa vyombo vya sheria vya Afrika Kusini.

Tangu Ijumaa, vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinaeleza kuhusu kuondoka kwa rais wa Sudan, Omar Al Bashir, ambaye aliondoka nchini Afrika Kusini Juni 15, bila hata hivyo kutaarifu vyombo husika.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya afrika Kusini, inasadikiwa kuwa mpango wa kumtorosha rais wa Sudan, ulipangwa kitambo ili asiwezi kuwa na wasiwasi. Ndege yake iliendeshwa kwa makini hadi kwenye kambi ya jeshi na kikosi cha ulinzi wa rais kiliombwa kishindikize hadi katika ndege yake.

Vyombo vya habari vimesema, bila hata hivyo kutaja jina, vyanzo rasmi. Kwa mujibu wa Phumla Williams, msemaji wa serikali, taarifa hii imeshapitwa na wakati.

“ Tunafutilia mbali taarifa zinazosema kuwa kuna mkutano uliyofanyika, kwa hiyo tutawasilisha ripoti yetu ya uchunguzi, kama ilivyotuomba Mahakama ya Pretoria. Hakuna jaribio lolote, kutoka kwetu kwa kuficha chochote kile. Walituomba tufanye uchunguzi , na ndivyo tunafanya, na tutatekeleza ahadi zetu ”, amesema Phumla Williams.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.