Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-BASHAR-ICC-SHERIA

Upinzani waomba uchunguzi kuhusu kushindwa kukamatwa kwa Bashir

Upinzani nchini Afrika Kusini unataka uchungunzi kufanyika kubaini ni kwanini serikali haikumkamata rais wa Sudan Omar Al Bashir na kumsafirisha katika Mahakama ya ICC mjini Hague.

Fatou Bensouda (kushoto), mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Hague na  Omar al-Bashir, rais wa Sudan.
Fatou Bensouda (kushoto), mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Hague na Omar al-Bashir, rais wa Sudan. AFP/Isaac Kasamani/Khaled Desouki/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Democratic Alliance kimesema kinataka kiongozi wa mashtaka kuweka wazi majina ya maafisa wa serikali walioamuru rais Bashir kupewa ulinzi na kufanikiwa kuondoka.

Gazeti la Sunday Times limeripoti kuwa mawaziri walikutana katika kikao cha siri na kuamua kuwa Bashir anarudi jijini Khartoum salama baada ya kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika jijini Johannreburg.

Rais Omar Al-Bashir alijielekeza wiki mbili zilizopita nchini Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa 25 wa Umoja wa Afrika ambao ulifunguliwa Jumapili Juni 14 jijini Johannesburg. Zaidi ya marais hamsini walihudhuria mkutano huo.

Awali Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC) iliiomba serikali ya Afrika Kusini kumzuia rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anatuhumiwa na Mahakama hiyo makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari katika vita viliyotokea Darfur.

Mahakama ya Afrika Kusini, iliombwa na shirika lisilo la kiserikali la Southern Africa Litigation Center, kumzuia rais wa Sudan ili asiwezi kuondoka nchini humo, angalau mpaka Jumatatu wiki hii.

Shirika hilo liliiomba Mahakama ya Afrka Kusini kumzuia rais Omar al-Bashir na kumsafirisha hadi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC). Kufuatia ombi hilo, Mahakama ya Pretoria ilikua ilimzuia rais wa Sudan kutothubutu kuondoka nchini Afrika Kusini mpaka vyombo vya sheria vitoe uamzi wake wa mwisho.

Waziri ya mambo ya ndani wa Afrika Kusini alikua alitakiwa kufuatilia kwa karibu maeneo yote hususan mipaka ambapo rais Omar al-Bashir anaweza kupitia kwa kuondoka nchini Afrika Kusini usiku wa Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.