Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-CHIBOK

Nigeria: Mmoja wa wanafunzi wa Chibok apatikana

Kwa mujibu wa jeshi la Nigeria na viongozi wa baadhi ya mashirika nchini Nigeria, mmoja wa wanafunzi wasichana 219 waliotekwa nyara mwaka 2014 na wapiganaji wa Boko Haram katika kijiji cha Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria alipatikana salama Jumanne hii Mei 17.

Picha ya Amina na mwanae iliyopigwa miezi michache na jeshi Maiduguri.
Picha ya Amina na mwanae iliyopigwa miezi michache na jeshi Maiduguri. © Nigeria Military
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Serikali ya Nigeria, Garba Shehu, amesema msichana huyo, aliyeokolewa hivi karibuni kutoka mikononi mwa Wanamgambo wa Boko Haram, atakutana na Rais Muhammadu Buhari na kupata msaada wa kuweza kujiunga na jamii yake.

Hata hivyo aliachiwa huru akiwa na mtoto mchanga. Jeshi la Nigeria limesema limemkamata mfuasi wa Boko Haram ambaye anasadikiwa kuwa ni mume wa msichana huyo.

Kwa mujibu wa kiongozi wa vuguvgu lililoanzishwa kwa minajili ya kuishawishi serikali kuwajibika kuwatafuta wasichana hao "BringBackOurGirls", msichana aitwaye Amina Ali alipatikana Jumanne hii Mei 17 katika msitu wa Sambisa katika jimbo la Borno. Alichukuliwa na kurejeshwa kijijini mwake Mbalala karibu na kijiji cha Chibok, na maafisa wa ulinzi wa msitu wa Sambisa, ambao wamedai kumuokoa msichana huo na kusema kuwa wanawasaidia wanajeshi wa Nigeria katika mapambano dhidi ya Boko Haram.

"Tunathibitisha kwamba mmoja wa wanafunzi wasichana wa shule ya Chibok waliotekwa nyara, aliokolewa na kikosi chetu, " Msemaji wa jeshi la Nigeria, Kanali Sani Usman, amesema katika taarifa yake, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

"Ameungana na wazazi wake, ambao wamembua kabla ya kupelekwa katika kambi ya jeshi ya mjini Damboa," Ayuba Alamson mmoja wa viongozi wa kiukoo wa Chibok.

"Baba yake anaitwa Ali na yeye anaitwa Amina. Niawatambua vizuri kwa sababu nilifanya kazi pamoja nao kama msemaji wa familia ya wasichana wa Chibok, " Alamson ameongeza.

Kiongozi wa shirika la Wazazi wa wasichana wa Chibok waliotekwa nyara, Yakubu Nkeki, pia amethibitisha jina la msichana na amesema msichana huyo alikuwa na umri wa miaka 17 wakati alipotekwa nyara tarehe 14 Aprili 2014. "Ni binti wa jirani yangu, walimleta nyumbani kwangu, " Yakubu Nkeki amesema.

Wasichana wengine wa Chibok bado wamesalia katika msitu wa Sambisa, ambapo jeshi la Nigeria limekua likiendelea na operesheni ya kuwatafuta wasichana hao kwa wiki kadhaa, wamesema viongozi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.