Pata taarifa kuu
MTAFARUKU-SIASA

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma asimamishwa kwenye chama cha ANC

Chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini kimetangaza siku ya Jumatatu kuwa kimemsimamisha kwenye chama rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma, ambaye alibainisha mwezi uliopita kuwa atafanya kampeni kwa niaba ya chama kingine kwa kuzingatia uchaguzi ujao.

Jacob Zuma, Julai 4, 2021 huko Nkandla.
Jacob Zuma, Julai 4, 2021 huko Nkandla. AFP - EMMANUEL CROSET
Matangazo ya kibiashara

 

"Zuma na wengine ambao mwenendo wao unakinzana na maadili na kanuni zetu watajikuta nje ya chama cha African National Congress" (ANC), amesema Fikile Mbalula, katibu mkuu wa ANC, ambayo inaongoza nchi tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Uamuzi huo unaotarajiwa na wengi ni ishara zaidi ya mgawanyiko ndani ya chama hicho katika unapokaribia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka huu - tarehe ya mwisho bado haijatangazwa lakini unatazamiwa kufanyika kati ya mwezi wa Mei na Agosti. Kutokana na kutawaliwa na kashfa za ufisadi katika mazingira magumu ya kijamii na kiuchumi, ANC, kwa muda mrefu ikikabiliwa na sintofaamu, inaweza kupoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza katika historia yake, kulingana na uchunguzi wa maoni.

Jacob Zuma alikuwa rais wa nne aliyechaguliwa kidemokrasia Afrika Kusini, kuanzia mwaka 2009 hadi 2018, lakini alilazimika kuondoka madarakani kwa sababu ya kesi za ufisadi na akatofautiana na chama alichokiongoza. Mwezi Desemba, Bw. Zuma, 81, alisema atafanya kampeni kwa ajili ya chama kipya kidogo chenye itikadi kali, Umkhonto We Sizwe (MK), kilichopewa jina la mrengo wa kijeshi wa ANC wakati wa kipindi cha ubaguzi wa rangi.

Fikile Mbalula ameongeza kuwa ANC itawasilisha malalamiko katika mahakama ya uchaguzi ili chama kipya kifutiwe usajili, na kuanzisha utaratibu wa kurejesha jina lake. "Kuundwa kwa chama cha MK sio bahati mbaya," amesema Bw. Mbalula baada ya mkutano wa kamati kuu ya ANC, uliohudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. "Hili ni jaribio la makusudi la kutumia historia ya kujivunia ya mapambano ya silaha dhidi ya utawala wa kibaguzi ili kutoa uaminifu kwa kile ambacho ni ajenda ya wazi dhidi ya mapinduzi," ameshutumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.