Pata taarifa kuu

Ajali ya ndege nchini Nepal: Wachunguzi wa Ufaransa watumwa kwenye eneo la tukio

Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Uchunguzi na Uchambuzi ya Ufaransa (BEA) kwa ajili ya usafiri wa anga inatarajiwa kuwasili Nepal siku ya Jumanne ili kushiriki katika uchunguzi wa ajali ya ndege yenye chapa ATR-72 ya shirika la ndege la Yeti Airlines siku ya Jumapili.

Kwa siku ya pili wanajeshi na wafanyakazi wengine, walikuwa wakiendelea kukusanya mabaki ya ndege hiyo, iliyokuwa itumie dakika 27 pekee kutoka Kathmandu hadi kwenye mji wa Pokhara.
Kwa siku ya pili wanajeshi na wafanyakazi wengine, walikuwa wakiendelea kukusanya mabaki ya ndege hiyo, iliyokuwa itumie dakika 27 pekee kutoka Kathmandu hadi kwenye mji wa Pokhara. AP - Yunish Gurung
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi wa uokoaji nchini Nepal, wanaendelea na zoezi la kutafuta miili ya watu wanne ambao hawajapatikana baada ya ajali ya ndege iliyokuwa na abiria 72, mamlaka zikisema hakuna matumaini ya kupata walio hai.

Hadi sasa miili ya watu 68 ilikuwa imepatikana kati ya watu 72 walioorodheshwa kusafiri na ndege hiyo aina ya ATR 72 ya shirika Yeti.

Wafanyakazi wa uokoaji tangu jana walikuwa wakijaribu kukabiliana na hali mbaya ya hewa katika eneo ambako ndege hiyo ilianguka, wataalamu wakisema zoezi limekuwa gulu kutokana na ukubwa wa bonde lenye karibu mita 300.

Kwa siku ya pili wanajeshi na wafanyakazi wengine, walikuwa wakiendelea kukusanya mabaki ya ndege hiyo, iliyokuwa itumie dakika 27 pekee kutoka Kathmandu hadi kwenye mji wa Pokhara.

Kiongozi wa operesheni za uokoaji kwenye eneo la tukio, amesema wataendelea kuitafuta miili iliyosalia, huku maiti zilizopatikana zitafanyiwa uchunguzi wa kisayasi kwa utambuzi kabla ya kukabidhiwa kwa familia zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.